WABUNGE WALIOPIGANA MWEZI JANA KUTAKIWA KUCHANGIA TAULO ZA KIKE ELFU 23000 ILI KUSAIDIA JAMII

📌SAIDA ISSA 

PROMOTA wa Lady In Red  Mbunge wa Viti Maalum Sophia Mwakagenda ametoa shukrani kwa Wabunge waliopigana katika pambano lililofanyika mwezi mmoja uliopita Jijini Dodoma kutokana na pambano hilo kuchangia Taulo za Kike elfu 23000 huku akitoa wito kwa jamii kusaidiana.

Mhe. Mwakagenda ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akitoa Tuzo kwa washiriki waliopigana katika pambano hilo ambapo aliwaasa watu wenye uwezo kuwasaidia watu wenye saratani na watoto wa kike, ili kuwapa mahitaji mbalimbali zikiwemo taulo za kike.

Aidha Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kigoma Sylvia Sigula amesema yeye kama mwakilishi wa wananchi anapenda kutumia jina lake katika kujitengezea nafasi nzuri kwenye jamii hata hivyo alipambana katika pambano hilo kutokana na ajenda ya kuwasaidia wasichana pamoja na wanawake.

Hata hivyo Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Mhe.Salome Makamba ametoa wito kwa watu wenye majina makubwa kutumia majina yao katika kuisaidia jamii pia alijitoa kwa watoto wa kike kutokana na kupoteza zaidi ya siku 40 kutokwenda shuleni hata hivyo amewapa moyo wanawake wenye lengo la kuingia kwenye mchezo huo kutokana na kuzingatia taratibu zote za kiusalama.

 

Post a Comment

0 Comments