JWTZ LATOA KATAZO LA UVAAJI WA NGUO ZA KIJESHI

 ðŸ“ŒAISHA SULEYMAN

KAIMU Mkurugenzi wa habari na uhusiano makao makuu ya Jeshi JWTZ Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda ametoa katazo la uvaaji wa nguo za kijeshi jana wakati akizungumza na wandishi wa habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dodoma

Amesema kuwa mavazi hayo ni pamoja  na Kombati (vazi la mabaka mabaka) Makoti, tisheti, suruali, magauni, kofia, viatu mabegi na kaptula zenye rangi zinazofanana au kushonwa katika mitindo ya kijeshi 

Ameongeza kwa kusema katazo hilo ni kwa mujibu wa kifungu cha 99 cha Sheria ya ulinzi wa taifa (NDA) sura ya 192 Sheria namb 24 ya mwaka 1996 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Aidha ameongeza kwa kusema  kifungu cha 178 cha Sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 (Penal code) na kifungu cha 6 cha Sheria ya usalama wa taifa vinakataza raia kuvaa sare na mavazi ya majeshi ya ulinzi au yanayofanana nayo

Ndio maana tunatoa siku saba kujisalimisha bila kuchukuliwa hatua ili kuepuka usumbufu na jeshi na ambaye hatayawasilisha atakuwa na nia ovu na dhamira mbaya 

Ilonda 

Hata hivyo amesema zipo baadhi ya taasisi zinazowashonea watumishi wake sare aina hiyo, wapo pia wafanyabiashara wanaoingiza nchini mavazi ya aina  hiyo na kuyauza kwa baadhi ya raia kupitia katika maduka au maeneo yao ya biashara

JWTZ linaomba kupitia kwenu kuwafahamisha wananchi kuwa utekelezaji wa majukumuu yake ya msingi na mengineyo tunagemea sana ushirikiano mzuri na wananchi wote  pia  limeongeza kwa kusema  sio hekima kwetu kulumbana kwa namna yoyote ile na baadhi ya wananchi wenye mavazi yaliyokakatazwa

Wapo baadhi ambao kwa kuyatumia mavazi hayo wamekuwa wakitapeli wanachi na wengine kufanya vitendo viovu ambao pia wamekuwa wakidhaniwa kuwa ni wanajeshi 

Ilonda

 

Post a Comment

0 Comments