EMBIID KWENYE VIATU VYA MVP

 ðŸ“ŒCARLOS CLAUDIO

JOEL Hans Embiid ni mchezaji wa kikapu anayeshiriki ligi kuu ya kikapu nchini Marekani maarufu kwa jina la NBA. Mchezaji huyo aliyezaliwa nchini Cameroon mwenye uraia pacha wa Ufaransa na Marekani anayekipiga katika klabu ya Philadelphia 76ers amezidi kutamba na tuzo yake ya mchezaji bora ijulikanayo kama MVP (Most Valuable Player) ya mwaka 2023 baada ya kuwapiku wachezaji kama Nikola Jovic, Giannis Antetokounmpo, Luka Doncic, Jayson Tatum, Ja Morant pamoja na Lebron James ambao walikuwa katika kinyang’anyiro cha tuzo ya MVP.

Akizungumza na vyombo vya habari alisema ni ndoto kwake kupokea tuzo kubwa kama hiyo na imekuwa furaha kubwa kwa familia pamoja na kuleta heshima kwa klabu yake pamoja na kuongeza morali kwa wachezaji wenzake na anachukulia kama nyongeza ya tuzo na ndoto zake sasa ni kushinda kikombe cha ligi kwani timu ina wachezaji wazuri wanaomzunguka na kila mtu yupo tayari kuonja furaha ya kutwaa ubingwa wa NBA.

Mchezaji huyo aliongezea kwa sasa yupo vizuri kiafya na baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi ya kikapu ameelekezea nguvu zake kufanya mazoezi binafsi pia amesema katika kipindi hiki cha mapumziko anatarajia kuwa karibu na mke wake Anne De Paula ambaye amefunga nae ndoa tarehe 22 Julai 2023 na mwanamke huyo mwanamitindo wa Brazil mwenye makazi yake New York nchini Marekani.

Mchezaji huyo aliyewahi kukipiga katika timu ya Kansas Jayhawks amefunguka yupo tayari kutoa tamko juu ya chaguo la timu ya taifa ambayo ataitumikia kwenye mashindano ya kimataifa ila amesema mara baada ya mashindano ya kimataifa ya FIBA kutamatika Septemba 2023.

Kuhusiana na usajili wala sina shaka kwani tetesi zinazoendelea za mimi kutimkia Oklahoma City Thunder ni za uzushi, mimi nina mkataba wa miaka minne na 76ers ambao unatarajia kuisha 2026 na ninafuraha ndani ya klabu yangu pia bado tuna malengo ya muda mrefu na kocha Glen Antony (Doc Rivers)

Embiid.

Embiid anayejulikana kwa jina la utani `The Process’ aliyeibuka mfungaji bora kwa kuongeza idadi ya vikapu vingi kwa misimu ya miaka miwili mfululizo 2021-2022 na 2022-2023 na kujinyakulia tuzo ya NBA Scoring Champion akiwa ni kiungo wa kwanza kufanya hivyo tangu Shaquille O’Neal mnamo mwaka 2000 na kiungo Moses Malone mnamo mwaka 1982 akiwapiku wote kwa zaidi ya pointi 30 kama raia wa kigeni.

 Awali wakati wa uteuzi wa mchezaji huyo bora wa NBA iliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya NBA jijini New York nchini Marekani kutokana na idadi ya kura za wajumbe kutangaza rasmi na kamishina mkuu wa NBA Adam Silver saa chache huku Embiid akiwa katika maandalizi ya mchezo wa 3 timu yake Philadelphia 76ers ikiwa katika raundi ya pili ya playoff series dhidi ya Bolton Celtics katika uwanja wa nyumbani wa Wells Fargo Center wenye idadi ya mashabiki 21,376 waliosimama kwa shangwe na kumlaki mchezaji huyo machachari.

Post a Comment

0 Comments