LA PATRONA FC NDANI YA NDONDO CUP 2023

 ðŸ“ŒCARLOS CLAUDIO

TIMU ya soka ya La Patrona Fc yenye makazi yake kata ya Nkuhungu jijini Dodoma imeweza kukutanisha menejmenti ya timu pamoja na mashabiki wake katika ukumbi wa La Patrona Lounge uliopo kata ya Nkuhungu Kanisani kwa lengo la kujua makundi yaliyopangwa ya Ndodo Cup Clouds 2023 na timu yao imeangukia mikononi wa timu gani

Katika hatua hiyo ya makundi inayotarajia kuanza tarehe 10 Septemba,2023 na kabumbumbu litasakatwa katika viwanja vya Shell Complex Chamwino, Shule ya msingi Chan’gombe pamoja na dimba la Mtekelezo.

Akizungumza na CPC BLOG Afisa Habari wa timu ya La Patrona Fc Siaba Kilo amesema amefurahishwa na uitikio mkubwa wa mashabiki pamoja na vyombo vya habari katika tafrija fupi kwa malengo ya kuimarisha timu yao ya La Patrona Fc.

Alisema licha ya changamoto zinazowakabili bado wapo imara kuanzia katika bodi ya timu hadi wachezaji wao kwa lengo la kupambania maendeleo na mwendendo mzuri wa timu, mashabiki pamoja na wadau wanaowazunguka.

Kama tunavyojua timu yoyote inatakiwa kuwa na viongozi na timu yetu inaundwa na viongozi kadhaa akiwemo mwenyekiti, mwenyekiti msaidizi wa timu, mtendaji mkuu wa timu C.EO, muweka hazina wa timu na viongozi wengine mbali mbali kwa lengo la kuifikisha timu kileleni.

Malengo yetu sio kuishia Clouds Ndondo Cup bali malengo yetu ni mapana ikiwezekana kushiriki ligi ya mkoa, ligi daraja la tatu, ligi daraja la pili, championship na Mungu akitusaidia tutafika hadi ligi kuu kwa kutegemea nguvu na jitihada za viongozi.

Clouds Ndondo Cup 2024 tumekuja kivingine na kauli mbiu ya msimu huu kwa timu yetu Lapatrona Fc na tukisema ‘Lapatrona Football Club tunaitikia Burudani ziendelee’

Pia alisema nawashukuru sana wageni rasmi ambao ni afisa habari Peter Nchimbi kutokea timu ya King Stone pamoja na Abdilahi Selemani mtendaji mkuu wa Gwasa Fc kwa kuitikia wito wa mualiko kwani kufika kwenu kunaonesha ni jinsi gani tunavyoboresha mshikamano ndani ya timu zetu”. alisema Kilo.

Kwa upande wa muweka hazina wa timu ya Lapatrona Fc Mbwana Hashim alisema anawahakikishia wanachama wa klabu kuwa atazitunza pesa na kuhakikisha matumizi yote ya ndani na nje ya timu yatakuwa na manufaa ya kujenga na sio kubomoa kwani tuna nia nzuri na timu yetu pia tunaipenda sana kwa malengo ya kufikisha mbali.

Muweka hazina aliongezea kwa kusema safari hii wamefanya usajili ndani na nje ya mji wa Dodoma na katika bajeti yao watahakikisha kila mchezaji atalipwa kwa wakati na malipo hayo yataongezeka kadiri ya kiwango cha mchezaji kwa jitiada anazoonesha na kiwango bora, Pia ameweka hadharani bajeti yao ya kila mechi itakuwa sio chini ya milioni tatu.

 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments