MKUU WA WILAYA DODOMA ATOA USHAURI KWA WANANCHI KUFANYA MAZOEZI

📌AISHA SULEYMAN

MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mhe  Jabir Shekimweri amewaasa watu kufanya mazoezi ili  kuepukana na magonjwa yasiyo ambukizwa ambayo yamekuwa tishio kubwa katika maisha.

Shekimweri ameseyasema hayo Jijini Dodoma wakati akishiriki Bonanza lililoandaliwa na benki ya NMB, ambapo amesema michezo ni muhimu na husaidia kuweka mwili katika hali nzuri.

Mh Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kipindi hicho  aliasisi utaratibu wa kufanya mazoezi kwa pamoja ili kuweza kujenga tabia ya watu kufanya mazoezi.

Shekimweri

Aidha ameongeza kuwa magonjwa yasiyo ambukizwa kwasasa yamekuwa yakiongezeka kwa siku za hivi karibuni  na yamekuwa yakiwaathiri  watu kwa kiasi kikubwa.

Shekimweri ameendelea kwa kusema namna pekee ya kuepuka gharama ambazo mtu angetumia kwenye matibabu ya magojnwa hayo ni kujielekeza katika shughuli za maendeleo.

Namna bora ya kufanya mwili ukae sawa ni pamoja na kufanya mazoezi ili kuweza kutoa jasho kwawingi pia inasaidia  kuepuka magonjwa yasiyo ambukiza 

Shekimweri 

 

Post a Comment

0 Comments