PROMOTA MWAKAGENDA AJA NA WANYAMA BIG FIVE KWENYE MCHEZO WA NGUMI

 ðŸ“ŒSAIDA ISSA

PROMOTA kutoka Red Promotion ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Sophia Mwakagenda Leo Nov 2, 2023 Jiji Dodoma amemtambulisha pambano lake lingine kati ya Bondia Dullah Mbabe na Eric  Katompa kutoka Nchini DRC

Mhe. Mwakagenda amesema kuwa pambano hilo litafanyika Nov 25, 2023 Jijini Arusha lengo na madhumuni ya pambano hilo kufanyika Jijini humo ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kutangaza Utalii Kupitia makala yake ya Royal Tour

Kupitia royal tour ambayo Rais Samia aliitangaza na tukaona matokeo yake makubwa Mimi kama promota wa ngumi nimeona ni vyema kuja na  Big 5 ili kuweza kuendelea kuutangaza utalii wa Tanzania kupitia mchezo wa ngumi

Tumechagua wanyama wa Big 5 na hii itaenda kufuatia ushindi wa mtu na mshindi atachagua anataka kuwa mnyama gani baada ya kushinda pambano,"amesema.

Aidha Mhe. Mwakagenda amesema katika pambano hilo mshindi atapatiwa nafasi ya kuchagua jina la mnyama kutoka katika wanyama watano wakubwa

Mhe. Mwakagenda ameongeza kwa kusema kuwa watafuatilia kuona kama wasanii wanaotumia majina ya wanyama kama wameyasajili ili kuepuka mkanganyiko na wasanii hao pale watakapowapa majina hayo mabondia wao

 

Post a Comment

0 Comments