SERIKALI IMEVITAKA VYOMBO VYA HABARI KUFUATILIA KWA UMAKINI MAFUNZO YA KANUNI ZA UCHAGUZI

 ðŸ“ŒPENDO MANGALA

SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ,imevitaka  vyombo vya habari kufuatilia kwa umakini mafunzo ya kanuni za uchaguzi  katika kuelekea uchaguzi Mkuu wa Serikali za Mitaa kwani vina wajibu wa kutoa taarifa sahihi kwa Wananchi ili uchaguzi uwe wa amani.

Hayo yameelezwa leo February 13,2024 Jijini Dodoma na Naibu waziri wa Wizara hiyo kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mhandisi Mathew Kundo wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji Nchini ulioenda sambamba na kilele cha maadhimisho ya  siku ya Utangazaji Duniani

Mhandisi Kundo amebainisha kuwa katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa Vyombo vya Habari vinatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuzingatia Maadili na kanuni za utoaji Habari kwa jamii kwa maslahi ya Taifa.

Vyombo vya habari vina wajibu mkubwa katika Taifa letu hivyo ni muhimu kila mmoja kuzingatia taaluma na kutimiza majukumu yake kwa weledi mkubwa

Naibu Waziri

Pamoja na hayo ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, kuhakikisha inajitathmini Mara kwa Mara ili kürzt kukuza ni wapi kuna mapungugu na kuweza kufanya kazi mapungugufu hayo.

Ni muhimu sana kwenu TCRA kuliangalia suala hili kwa umakini mkubwa kwani Mkifanya hivi itawasaidia  sana kufanya kazi kwa ufanisi, na Sisi kama Serikali tunawaahidi kuendeleza ushirikiano uliopo ili kuleta maendeleo kwa jamii

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ( TCRA) Jones Kilimbe amewataka watangazaji na waandishi wa habari kuzingatia Madili na kanuni ya kazi zao.

Kilimbe pia amezungumzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwa, vyombo vya habari vina jukumu la kutoa elimu kwa wapiga kura ikiwa ni pamoja na kuhabarisha umma kuhusu mwenendo mzima wa kampeni bila upendeleo na kutoa ripoti sahihi za siku ya kupiga kura. 

Amesema TCRA kama wadau wa Utangazaji watahakikisha wanakuwa bega kwa bega na vyombo vya Utangazaji kwa kuhakikisha wanatoa mwelekeo wa maudhui yenye ubora bila upotoshaji. 

Maudhui ya Utangazaji ni chakula kwa jamii, yanaweza kujenga au kubomoa, kuharakisha maendeleo au kukwamisha hivyo ni jukumu la vyombo vya Utangazaji kujikita katika kuhabarisha umma maeneo yenye tija na kuachana na uchochezi au uvunjifu wa Madili

Naye Mwenyekiti  wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini( MOAT) Samwel Nyala amesema pamoja na kukuza tasnia  ya habari  bado kuna changamoto mbalimbali ikiwemo gharama kubwa ya  leseni hali inayowakwambisha na kuwapa hasara ya uendeshaji . 

Kutokana na hilo, Nyala  ameiomba Serikali  kuangalia suala hilokwa kina nakuomba ruzuku kwa Vyombo vya Habari kutokana na kuwepo kwa mdororo wa Uchumi.

Kwa upande wake mdau wa Habari kutoka Chama cha watangazaji (NIBA) Amos Ngosha ameeleza masikitiko yake kuhusu hali ya uchumi wa vyombo vya habari kuwa imedorora kutokana na kukosa ruzuku kutoka Serikalini. 

Ametumia nafasi hiyo kuitwka Serikali kuanza kutoa ruzuku kwa vyombo vya habari ili viweze kujiendesha. 

Tunashindwa kujiendesha kwa kukosa matangazo, matangazo yetu yamekuwa ni ya waganga wa tiba asili na viongozi wa dini,tunatozwa Kodi kubwa kuliko faida tunayoipata, tunaomba taaluma hii iheshimiwe  kwa kutupunguzia gharama za uendeshaji


 

Post a Comment

0 Comments