MIKUTANO YA BARAZA LA WAFANYAKAZI LITUMIKE KUJADILI MALENGO NA MIPANGO YA TAASISI - MHE. NDEJEMBI.

📌ABDULKARIM KESSY

NAIBU Waziri ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya elimu Deogratius Ndejembi amesema mikutano ya baraza la wafanyakazi itumike kujadili malengo na maslahi ya watumishi ili kuwepo na matokeo bora ya kiutendaji kazi katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

Akizungumza leo Machi 12, 2024 jijini Dodoma, Mhe. Deo Ndejembi amesema mabaraza ya wafanyakazi yanatakiwa kujadili utendaji kazi wa kila siku na jinsi ya kuboresha utendaji pamoja na umuhimu wa kila mtumishi katika taasisi kufahamu malengo ya taasisi husika.

Lengo la kikao hiko ni kujadili taarifa na maswala yanayohusu mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024, mapendekezo ya mpango wa bajeti ya ofisi ya Rais TAMISEMI ya mwaka wa fedha 2024/2025 pamoja na mada kuhusu vyama vya wafanyakazi yatakayotolewa na ofisi ya waziri mkuu kazi.

Tija na masilahi lazima viwe na uwiano ili kuwa na matokeo bora ya utendaji kazi unaolenga kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi aidha niwakumbushe kuwa hakuna haki bila malipo hivyo ieleweke kuwa utendaji bora wa kazi na wenye tija kwa kuzingatia weledi na uwajibikaji utawezesha serikali kuongeza mapato na hivyo kuwezesha kuongeza utoaji wa masilahi bora

Mhe. Djejembi.

Amesema ofisi ya Rais TAMISEMI ndio ofisi inayogusa maisha ya wananchi katika kila sekta inayotekeleza majukumu katika mikoa 26, wilaya 139, halmashauri 184, tarafa 570, kata3956, mitaa 4263, vijiji 12319 na vitongoji 64384.

Wajumbe wote mnao wajibu na jukumu la kuhakikisha kwamba malengo, mipango na bajeti ya wizara inatekelezwa na kufikiwa kama ilivyopangwa, Usimamizi na utekelezaji wa mpango wa bajeti ni jukumu letu sote, tushirikiane na kuhakikisha kwamba malengo yetu yanafikiwa kuanzia katika idara,vitengo, taasisi na hatimae katika umoja wetu kama ofisi ya Rais TAMISEMI ili kuhakikisha kuwa huduma bora zinawafikia wananchi kwa lengo la kuwaletea maendeleo.

Pia ametoa pongezi kwa kazi iliyofanyika katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 ikiwa usimamizi na ufuatiliaji wa ujenzi wa majengo ya utawala katika mikoa, halmashauri, tarafa, kata, mitaa na vijiji, usimamizi na ufuatiliaji wa ujenzi wa hospitali za wilaya na vituo vya kutolea huduma za afya, uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza kutokana na sera ya elimu bure pamoja na hali ya ufaulu ya wanafunzi wa darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita kuongezeka.

Amesema taasisi za ofisi ya Rais TAMISEMI mikoa na mamlaka ya serikali za mitaa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 hadi kufikia Februari, 2024 zimekadiria kukusanya mapato ndani ya halmashauri kupitia vyanzo mbali mbali kama vile ushuru wa mazao, ushuru wa huduma, vibali, ushuru wa masoko, ada za uchangiaji huduma za afya kulingana na mapato lengwa ya halmashauri husika na kufanikisha kukusanya zaka 64.91% ya malengo yaliyowekwa.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Dkt. Charles Msonde amesema baraza la wafanyakazi liliundwa kama ilivyo mabaraza mengine ya wafanyakazi katika maeneo mengine kwa muujibu ya sheria ya mwaka 2003 kifungu cha 30 kifungu kidogo cha 3 ambacho kilianzisha uwepo wa mabaraza ya wafanyakazi.

Amesema malengo ya kuanzisha baraza la wafanyakazi ni kuongeza tija na uwajibikaji miongoni mwa watumishi wa umma kwani ni daraja linalounganisha watumishi na menejimenti huku uwepo wa baraza hilo linaleta masuala mazuri pamoja na tija kazini katika kuleta ufanisi, utendaji kazi na kuhakikisha watumishi wanatekeleza wajibu wao kwa nidhamu wawapo kazini.

 


 

 

 

Post a Comment

0 Comments