TUMEUONA MWANZO NA MWISHO WA POUL POGBA

📌 ABDULKARIM KESSY

FEBRUARY 28,2028 itakuwa siku ya Jumatatu wazungu walituletea jina la 'Brue Monday'. Kama itaenda kama ilivyopangwa katika kifungo cha Poul Pogba basi ndio siku ambayo atakuwa anamaliza kifungo chake cha kucheza soka.

Amefungiwa miaka minne na wahusika wa dawa za kuongeza nguvu michezoni. Kama ni kurudi atarudi akiwa na miaka 34. Kwa sasa ana umri wa miaka 30. Dunia imemuelemea Pogba sijui nini kitamtokea kwenye maisha mema yake ya soka.

Kifungo hiki ni msumari wa mwisho katika maisha yake ya soka, amedai kuwa atakata  rufaa yake ikishindwa basi huenda huu ndo ukawa mwisho wa maisha ya soka lake. Yeye sio wa kwanza kukutwa na hukumu kama hii.

Pogba sio wa kwanza kufungiwa kwa kosa hilo ikumbukwe wapo waliowahi kufungiwa tukianza na gwiji wa soka Diego Maradona, Deco, Andrew Onana, hao ni baadhi ya mastaa wa mchezo wa soka waliokutana na shutuma na hukumu za kosa hilo.

Kiungo wa Juventus na Ufaransa Poul Pogba amesimamishwa baada ya uchunguzi wa dawa za misuli kuonesha kiwango cha juu vya testosteron, (homoni inayoimarisha misuli na mifupa mwilini, ambayo inakatazwa na mamlaka husika),

Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya nchini Italia Nado imesema kuwa Pogba alikiuka sheria ya kupambana na dawa za kulevya kwani walipata tone la hiyo dawa iliyokatazwa "Metabolitize zisizo za asili ya Testosterone"

Klabu yake ya Juventus ilisema katika taarifa yake kuwa Pogba "aliarifiwa kusimamishwa soka kwa muda kwa tahadhari."

Klabu ina haki ya kuzingatia hatua zifuatazo kwa utaratibu," taratibu hiyo iliongeza. Ukaguzi wa kimatibabu ulihusisha sampuli "A" Na Pogba anakabiliwa na marufuku ya miaka minne ikiwa vipimo vya sampuli "B" pia itatoa matokeo chanya ya Testosterone. Kwa upande wake muwakilishi wa Pogba, Rafaela Pimenta alisema kwa ujumbe wake ya kuwa, alikuwa "akisubiri sampuli ya pili na hawezi kutoa maoni kabla ya matokeo.

Kwa uhalika ni kwamba Poul Pogba hakutaka kamwe kuvunja sheria

Pogba alihamia Juventus mnamo July 2022 kutoka Manchester United ya Uingereza, kuanzia 2012 hadi 2016 aliisaidia Juventus kushinda mataji manne ya Serie A na vikombe viwili vya Italia, na kuiwezesha kutwaa fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya mnamo 2015.

Pogba alikuwa Kiungo muhimu kwenye ubingwa wa kombe la Dunia 2018 lakini msimu wake wa 2022/23 uliathiriwa na majeraha pamoja na sakata ya mamilioni ya Euro ya uonevu iliohusisha marafiki zake wa utotoni na ndugu yake.

Aliwakilisha Juventus mechi 10 pekee katika msimu huo na hata kutocheza kombe la Dunia la 2022 na Ufaransa

Pogba alisema wakati mwengine alivunjwa moyo sana na jambo hilo.

Nilikuwa peke yangu nikiwaza kuwa sitaki kuwa na pesa tena, sitaki kucheza tena, nataka tu kuwa na watu wa kawaida, ili wanipende mimi kama mtu, sio kwa umaarufu sio kwa pesa

Pogba.

Baada ya kuvunjwa moyo hivi karibuni Pogba sasa anasubiri kwa matokeo ya uchunguzi wake wa sampuli "B" 

Post a Comment

0 Comments