TUME ya Ulinzi wa Taarifa
Binafsi (PDPC) imetekeleza agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la
kuhakikisha Taasisi zote za Umma na binafsi kuwa zimesajiliwa kwenye Tume hiyo
ifikapo Disemba 31,2024 ambapo mpaka sasa Taasisi zaidi ya 700 tayari
zimejisajili .
Hayo yamesemwa leo Novemba 25, 2024 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa PDPC Emanuel Mkilia wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea kwenye warsha ya kuongeza uelewa kwa maofisa wasimamizi wa taarifa binafsi kuhusu dhana ya ulinzi wa taarifa binafsi inayotarajiwa kufanyika Disemba 17,18 jijini Dar es salaam.
Akizungumzia kuhusu ulinzi wa taarifa za mtu binafsi Mkilia amesema sehemu yoyote ambayo mwananchi ataombwa taarifa zake zinatakiwa zitunzwe kwa kuwa zinatolewa kwaajili ya kutoa huduma, huku akiwataja wale wanaotoa mikopo mitandaoni.
Nae Dorothy Ndazi kutoka kampuni ya wanasheria ya Hilton Law Group amesema wameshirikiana na PDPC ili kuweza kupeleka uelewa kwa jamii kuhusiana na ulinzi wa taarifa binafsi.
0 Comments