SERIKALI YASISITIZA UMUHIMU WA TAKWIMU KATIKA ELIMU KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

 







📌BAHATI MSANJILA

Ikiwa leo ni siku ya Takwimu Afrika Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeadhimisha siku hiyo kwakuungana na wananchi wa Chamwino Dodoma pamoja na kutoa vifaa vya ujenzi wa jiko katika shule ya wanafunzi Wenye mahitaji Maalumu Buigiri.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Janeth Mayanja amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi ya kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalumu wanapata elimu bila kikwazo.

Ameipongeza NBS kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jiko la kupikia chakula cha wanafunzi hao na Walimu..

Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassa imeendelea kuiwezesha NBS kufanya kazi zake kwa weredi kwasababu ni ukweli usiopingika kuwa hakuna Taifa linaloweza kuendelea bila kuwa na Takwimu sahihi.

Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk.Albina Chuwa amesema katika kuadhimisha siku ya takwimu Afrika wameamua kutoa mchango wao wa ujenzi wa jiko kwa ajili ya kupika chakula cha wanafunzi wenye mahitaji maalumu 

Amesema mchango ilitolewa ni tofari 700, simenti mifuko 27, bati za rangi 25, mbao 24, misumari, rangi na fedha Kwa ajili ya fundi sh.500,000 vyenye jumla ya zaidi ya sh.milioni tatu

Dkt. Chuwa amesema katika kuadhimisha siku ya takwimu Afrika wameamua kuungana na watoto lengo ikiwa ni kuhamasisha matumizi ya takwimu katika kupanga mipango mbalimbali ya Maendeleo.

 







Post a Comment

0 Comments