LICHA
ya kuwepo kwa Rushwa ya ngono katika jamii, muamko wa wahanga wa ukatili kutoa
taarifa kwenye vyombo husika
umekuwa mdogo kutokana na wahanga hao kutotoa ushirikiano katika Taasisi ya
Kuzuia na kupambana na Rushwa
Mkuu
wa Dawati la uzuaija Rushwa kutoka TAKUKURU Mkoa wa Manyara Paschal Mhagama
amesema hayo wakati akiwasilisha mada inayohusu Rushwa za ngono na madhara yake
katika Uzinduzi wa Kampeni maalum ya siku 16 za Kupinga Ukatili wa kijinsia
iliyofanyika Mkoani Manyara
Amesema
kwa mwaka 2023 makosa ya Rushwa ya ngono yaliyolipotiwa ni 28 tu licha ya
kuwepo kwa vitendo hivyo, ambapo ameitaka jamii kutoa taarifa TAKUKURU
wanapokumbwa na Rushwa ya ngono
0 Comments