📌BAHATI MSANJILA
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi amesema lugha ya Kiswahili kutoka Tanzania imeendelea kukua na sasa imefikia kuwa lugha ya saba duniani, huku Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) likifungua vituo 17 katika mataifa mbalimbali duniani ili kuendelea kukuza lugha hiyo.
Prof. Kabudi ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wakati akizungumza kuhusu mafanikio ya wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na kubainisha kuwa ndani ya nchi tayari vimeanzishwa vituo 30 vinavyofundisha lugha ya Kiswahili.
Kwaupande wa Sekta ya michezo amesema Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 161. 977 kwaajili ya ujenzi na ukarabati wa viwanja vya mashindano ya mpira wa miguu kwa mataifa ya Afrika (AFCON) yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2027.
Akizungumzia Kuhusu kuziwezesha timu za taifa kufuzu na kushirki mashindano ya kimataifa waziri Prof.Kabudi amesema Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilion 8.5
Akizungumza jijini Dodoma, Prof. Kabudi amesema mafanikio hayo ni uthibitisho wa dhamira ya kweli ya Serikali ya kuwekeza katika maendeleo ya vijana, kukuza vipaji, na kuitangaza Tanzania kitaifa na kimataifa kupitia michezo, sanaa, utamaduni na lugha ya Kiswahili.
Akieleza kuhusu sekta ya utamaduni, Waziri Kabudi amesema Serikali imefanikiwa kuandaa matamasha matatu ya kitaifa ya utamaduni na kuendelea kusherehekea Siku ya Kiswahili Duniani kila Julai 7, baada ya Kiswahili kutambuliwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2024.
Prof. Kabudi amesema kuwa mafanikio mengine ni kuanzishwa kwa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari mnamo Machi 3, 2025, hatua inayolenga kudhibiti ubora wa kazi za habari, kuongeza weledi na kuimarisha maadili ya taaluma ya uandishi wa habari nchini.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita
inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu
Hassan, kwa mafanikio makubwa katika sekta ya habari, utamaduni, sanaa na
michezo ndani ya kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya sita.
0 Comments