DIWANI KATA YA PWAGA 'HOI' KURA ZA MAONI, WAJUMBE 'WAMFUNGIA VIOO'

Wilfred Elisha Mgonera aliyeongoza kura za maoni Kata ya Pwaga,Mpwapwa

📌NA BARNABAS KISENGI                                        

Diwani aliyemaliza muda wake katika kata ya Pwaga jimbo la Kibakwe Wilayani Mpwapwa Vicent Chawala ameshindwa kutetea kiti chake katika uchaguzi wa kura za maoni zilizofanyika mwishoni mwa wiki wilayani humo.

Katika Uchaguzi huo ambao Wilfred Elisha Mgonera aliibuka ‘kidedea’ kwa kuzoa kura 111, Chawala ameshika nafasi ya nne (4) amepata kura 15 kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo.

Nafasi ya pili imeshikwa na na Fadhili Mngoke aliyepata kura 22 na Harodi Mkombola akishika nafasi ya tatu kwa ‘kuzoa’ kura 21.


Wagombea wengine waliowania nafasi hiyo ni Fadhili amepata kura 15, Ashley Malolela (13), Henry Kishimu (12), John Madee  (6) na Steven Mtuta (1) na Julius Lugodi (0).

Post a Comment

0 Comments