WAKAZI WA MAHOMANYIKA 'WAMJIA JUU' MKANDARASI BARABARA ZA MJI WA SERIKALI

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mahomanyika Enerst Kutona akiongea
na Wakazi wa Mtaa huo waliofika eneo lenye mgogoro

Wananchi wa Mtaa wa Mahomanyika kata ya Nzuguni jijini Dodoma wameomba serikali kuingilia kati mgorogo unaendelea kati yao na kampuni ya ujenzi ya China Henan International Cooperation Group (CHICO) juu ya eneo la mgodi wa madini ya ujenzi liliopo katika mtaa huo.

Wananchi hao wanailalamikia kampuni hiyo kuvamia eneo katika mtaa huo na kuanza kuchimba na kuchukua mchanga (kifusi) kwa ajili ya ujenzi wa barabara katika mji mpya wa serikali (Mtumba).

Kwa mujibu wa Enerst Kutona ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa huo uliopo nje kidogo ya mji wa Dodoma amesema hawana taarifa kuhusu ujio wa kampuni hiyo na shughuli za uchimbaji wanzozifanya katika mtaa huo licha ya kupokea barua ya utambulisho.

Tulipokea barua kutoka TARURA ya kukutaka tuwape ushirikiano kampuni ya CHICO wakiwa wanatekeleza mradi wa barabara,lakini hatuna taarifa ya wao (CHICO) kufungua mgodi wa rasilimali za ujenzi
Enerst KutonaBarua waliopokea Serikali ya Kijiji kutambulishwa kwa mkandarasi.

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa wakazi wa mtaa huo wanachohitaji ni kujua wanafaidika vipi na eneo hilo maana kampuni hiyo itaacha mashimo katika eneo hilo baada ya ujenzi kumalizika.

Amesema licha ya kufanya jitihada mbali za wakuwasiliana na malamla zinazohusika kujua uwepo wa mgodi huo wa mchanga na kokoti kwa ajili ya ujenzi lakini hawajawahi kupata majibu.

Eneo ambalo kampuni ya CHICO inachimba mchanga katika mtaa huo

Nae Nyemo Kiswagala ambaye ni moja wa  wajumbe wa serikali ya mtaa huo amesema lengo lao kubwa ni kutaka kufahamu wao wanafaidika vipi na uwepo wa kampuni ya CHICO katika mtaa wao.

Lile eneo linachimbwa kifusi ni maeneo ya watu binafsi na ushahidi ni yale makaburi yaliyopo pale,kinachoniumiza CHICO hawajaja hata ofisini kujitambulisha na hata tulipowafuata wamesema hilo suala lipo chini ya TARURA ndio wanajua kila kitu na ukienda TARURA wanasema kazi wamempa CHICO yaani mwisho hatuelewi cha kufanya
Nyemo Kiswagala


Mwandishi wetu alifika eneo hilo linalochimbwa mchanga huo na kushuhudia baadhi ya wananchi wakiwa eneo hilo wakiomba ridhaa ya viongozi wao kuyazuia magari hayo yasiendelee na kusomba mchanga huo hadi suluhu itakapopatikana.

“Tunachotaka hapa wasitishe hii kazi kwa muda hadi tutakapokubaliana.Tunataka kujua nani amekubaliana na huyo Mchina (CHICO) aje kuvamia maeneo yetu na kuchimba kifusi wamefika kuanza kuchimba hadi makaburi bila makubaliano na wanakijiji”-Amsema Felix Aidan mkazi wa Mahomanyika.

Malori ya kampuni ya CHICO yakisomba mchanga kutoka eneo hilo lenye mgogoro

Kwa upande wake Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Ujenzi ya CHICO Isaack Adrian amesema wao hawahusiki katika sakata hilo.

Meneja huyo amesema wao walipokabidhiwa kazi hiyo mteja wao (TARURA) alienda kuwaonesha eneo hilo kwa ajili ya kupata mchanga (kifusi) kwa ajili ya kujengea barabara za mji wa serikali ambazo zina urefu wa kilomita 40.

Mwandishi wetu pia alifika katika ofisi za TARURA (Mtumba-Dodoma),akizzungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Taasisi hiyo (Alikuwa kwenye kikao cha bodi ya Manunuzi) Mhandisi Benjamini Magege amesema TARURA ina taarifa kuhusu mgogoro huo na wamejiandaa kukutana na pande zote akiwemo na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuona namna bora ya kutatua mzozo huo.


Post a Comment

0 Comments