"TUNAKWENDA KUWEKA REKODI UCHAGUZI MKUU 2020"- CHAMA CHA DP
📌NA HAMIDA RAMADHANI

CHAMA cha Democratic Part (DP)  kimesema kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu Chama hicho kinakwenda kuvunja rekodi kwa kushinda kwa kishindo na kushika dola .

Akizungumza na Wajumbe wa kwenye Mkutano Mkuu maalum wa wagombea watakaopeperusha bendera ya chama hicho kwa nafasi ya Rais na Makamu wa Rais Tanzania bara na Zanzibar Katibu wa chama DP, Abdul Mluya amesema malengo ya chama hicho ni kukamata dola.

Aidha Mluya ambaye pia ni mwenyekiti wa uchaguzi katika chama hicho amesema chama cha Demokratic Part kinakwenda kushinda na sio kuwakilisha kwasababu chama hicho ni kikubwa na kikongwe hivyo lazima kichukue dola .

Napenda itambulike kwamba hakuna chama kidogo cha siasa bali kunavyama dumavu vya siasa na mwaka huu lazima tuvunje rekodi kwa kuingia madarakani kwa kishindo.
Abdul Mluya.


Hata hivyo amewataja walioteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho kuwa ni pamoja na Philip John Fumbo ambaye anakwenda kupambana na Rais John Magufuli wa CCM na mgombea mwenza kwa nafasi ya Makamu wa Rais Zainabu Juma Khamis na mgombea urais Zanzibar Shafii Hassan Suleiman.
Mluya ametumia fursa hiyo kuiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iwatangaze pindi watakapopata ushindi na kwamba wao wapo tayari kumpa hongera mshindi atakayepata ushindi huo kihalali.

Watu huwa wanasema  sisi tunapenda kesi,hili tunasema kweli kwamba tupo tayari kufungua kesi hata elfu kumi kama hatutatendewa haki .
Abdul Mluya

Kwa upande wake aliyeteuliwa kupeperusha bendera ya urais kupitia chama chicho cha Demokratic Part Philip John Fumbo amesema kuwa kutokana na sera nzuri ya chama chao wanakwenda kushinda kwani watanzania wengi ni walala hoi na ndio sera ya chama chao.

Naye mgombea urais wa Zanzibar Suleiman amesema akipata nafasi ya kuwatumikia watanzania kwa upande wa Zanzibar atakwenda kutatua changamoto nyingi zinazowakabili wazanzibar kwa kutumia rasilimali nyingi walizonazo ikiwemo bahari.

Post a Comment

0 Comments