KUCHOMWA MOTO OFISI ZA VYAMA VYA SIASA KWA WASHTUA JUMUIYA YA MARIDHIANO,WAITISHA KONGAMANO LA AMANI



📌NA.FAUSTINE GIMU GALAFONI



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli anatarajia kuwa Mgeni Rasmi katika kongamano la kitaifa la Jumuiya ya Maridhiano litakalofanyika siku ya Jumatatu Agosti,24,2020  jijini Dodoma.


Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti,21,2020 jijini Dodoma,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania ambayo inahusisha dini zote za wailam na Wakristo,Sheikh Alhad Musa Salum amesema kongamano hilo litatoa fursa kwa viongozi wote wa dini kuwasihi wagombea  kufanya kampeni za busara zisizo na matusi,Pamoja na kuhamasisha tume ya Taifa ya Uchaguzi kusimamia haki ili kuendelea kutunza amani ya Tanzania.

Sisi watanzania ni watu wastaarabu saana hivyo hivyo katika kongamano hilo kutakuwa na miogozo mbalimbali hasa kuwahamasisha wanasiasa kufanya kampeni za busara zisizo na matusi pia tutatoa miongozo kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kusimamia Haki katika uchaguzi mkuu Oktoba 28 

Pia Sheikh  Alhad Musa Salum amesema ,katika Kongamano hilo la Amani la Jumuiya ya Maridhiano mambo mengine yatakayojadiliwa ni elimu kwa wananchi umuhimu wa ushiriki katika kupiga kura ambapo Zaidi ya wageni elfu kumi wanatarajia kuhudhuria katika kongamano hilo.

Hivyo,Sheikh Salum amesema sababu za kufanya kongamano hilo ni baada ya kuona viashiria vingi vya uvunjifu wa amani vikiwemo kuchomwa moto baadhi ya ofisi za vyama ,matusi na vijembe baadhi ya wagombea  ambapo pia amebainisha kuwa kundi la watu wenye ulemavu litapewa kipaumbele Zaidi katika ushiriki wa kongamano  hilo.



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Taifa, Sheikh Alhad Musa Salum

Kwa upande wake Katibu mkuu wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania,Askofu  Dkt.Osward Herman Mlay amesema kuna umuhimu kwa viongozi wa dini kuungana bila kujali itikadi za dini zao ambapo pia  ametoa onyo kwa viongozi wa dini wanaojihusisha na masuala ya kisiasa katika nyumba za ibaada kwani wanaweza kuhatarisha amani ya nchi.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano idara ya wanawake mkoa wa Dodoma Pili Mohammed Yomba amesema kamati katika mkoa wa Dodoma imejipanga kuwahudumia wageni wanaotoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.

Post a Comment

0 Comments