LISSU ATOA PINGAMIZI KWA JPM NA LIPUMBA


📌NA.FAUSTINE GIMU GALAFONI

MGOMBEA Urais kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu ametoa mapingamizi kwa wagombea wawili kiti cha Urais 

Akizungumza na Waandishi wa habari Leo Agosti 26,2020 jijini Dodoma Lissu ametaja waliowekewa pingamizi ni pamoja na mgombea Urais kupitia Chama  Cha Mapinduzi(CCM) Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgombea Urais kupitia Chama Cha Wananchi(CUF) Prof.Ibrahim Haruna Lipumba.

Miongoni mwa Mapingamizi aliyotoa Lissu ni pamoja na pingamizi la kurejesha fomu za wadhamini kabla ya tarehe ya uteuzi,pamoja ,kusainiwa fomu kwa wakurugenzi badala ya kusainiwa na tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na kuweka kuweka passport size isiyokidhi vigezo.

Hivyo,Lissu  amesema kwa mujibu wa sheria wawekewa pingamizi wanapaswa kukutana ana kwa ana na muweka pingamizi katika ofisi za tume ya Taifa ya uchaguzi jijini Dodoma kujitetea dhidi ya mapingamizi hayo.

Kuhusu suala la kukatwa kwa majina ya  wagombea udiwani na ubunge wa CHADEMA  Lissu amewataka kukata rufaa Mara moja  katika  ofisi za tume za majimbo  na ngazi za juu za ofisi za tume ya taifa ya Uchaguzi ili wapate fursa ya kujitetea.



Post a Comment

0 Comments