NEC YATUPILIA MBALI MAPINGAMIZI YA LISSU



📌NA HAMIDA RAMADHANI

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetupilia mbali mapingamizi mawili yaliyowekwa na mgombea urais kupitia Chama cha Demojrasia na Maendeleo(Chadema)Tundu Lissu dhidi ya wagombea wa nafasi hiyo Dkt.John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi na Profesa Ibrahim Lipumba wa Chamancha Wananchi (CUF).
Awali akizungumza na waaandishi wa habari katoka ofisi za Chadema jijini Dodoma kuhusu mapingamizi hayo Lissu amesema,ameweka mapingamizi mawili dhidi ya Rais Magufuli na pingamizi moja dhidi ya profesa Lipumba kwa madai kwamba hawajakidhi masharti na sheria za uchaguzi.
Lissu alitaja pingamizi la kwanza ambalo linamuhusu Dkt.Magufuli na Profesa Lipumba kuwa ni kupeleka fomu zao za wadhamini  kukaguliwa na kuhakikiwa na wakurugenzi wa uchaguzi na kisha kugongwa mihuri wakati wenye mamlaka ya kufanya hivyo ni NEC pekee yake kwa mujibubwa sheria za Tume hiyo.
Pingamizi la pili linamuhusu Dkt Magufuli peke yake ambalo amedai picha zilizoambatanishwa kwenye fomu zake siyo zilizohitajika kwa mujibu wa sheria za Tume ya Uchaguzi ambazo ni picha mdogo (paspot size) lakini mgombea huyo amesema picha zilizopigwa upande na kwamba kinachoonekana ni nusu sura.
Pingamizi la kwanza ni mgombea kupitisha fomu zake za kutafuta wadhamini kuhakikiwa na kugongwa mihuri na wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo aliowateua yeye na pingamizi hili pia linamuhusu Profesa Lipumba huku akisema ni kinyume cha sheria ya uchaguzi.
Tundu Lissu

Lissu amesema NEC ndiyo yenye Mamlaka ya kuhakiki wadhamini wote kutoka mikoa 10 Tanzania bara na mikoa miwili Tanzania Visiwani.

Kufuata mapingamizi hayo ameiomba NEC baada ya kuwapa muda wa kujitetea waliowekewa mapingamizi iwakutanishe muweka na wawekewa mapingamizi kwa mujibu wa sheria.



TUME YA UCHAGUZI YATOA MAJIBU
Akitoa uamuzi wa NEC, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Wilson Mahera amesema kuwa NEC  kwa kuzingatia masharti ya kanuni 39(5) ya kanuni za uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020, baada kupokea mapingamizi dhidi ya wagombea hao ,iliwataarifu mapema iwezekanavyo na wahusika wamewasilisha utetezi wao kwa Time hiyo.
Akizungumza mapingamizi dhidi ya Dkt.Magufuli kwamba hakuambatisha picha kwenye fomu za uteuzi na hakurudisha fomu ya utetezi kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na sheria, Dkt.Mahera amesema "Tume baada ya kupitia sababu za mapingamizi imejiridhisha kuwa Dkt.Magufuli amerejesha fomu zake ambazo zimeambatishwa pamoja na picha kwa mujibu wa sheria ,kanuni na maelekezo ya Tume ,
Hivyo imehiridhisha kwamba mapingamizi hayo hayana msingi wa kisheria  na kuyatupilia mbali na kwa maana hiyo Dkt.Magufuli ni mgombea halali wa kati cha Rais kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Dkt. Mahera
Kuhusu mgombea wa CUF Dkt.Mahera amesema kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na sheria,Tume baada ya kupitia sababu ya pingamizi pamoja na utetezi uliotolewa ,imejiiridhisha kuwa mgombea huyo kupitia Chama cha wananchi (CUF),amerejesha fomu zake kwa mujibu wa sheria ,kanuni na maelekezo ya NEC.
Hivyo NEC imejiridhisha kwamba pingamizi hilo halina msingi wa kisheria  na imelitupilia mbali na kwa hiyo Profesa Ibrahim Lipumba wanaendelea kuwa mgombea halali wa kati cha Rais kupitia Chama cha wananchi (CUF).
 Dkt.Mahera
Aidha alisema kwa mujibu wa kanuni ya 39(6) ya kanuni za uchaguzi wa  Rais na Wabunge za mwaka 2020 ,sababu za uamuzi huo wa Tume watapewa kwa maandishi wale wote walioweka pingamizi wa waliowekewa pingamizi.

Post a Comment

0 Comments