MBWANA SAMATTA AJIUNGA NA KLABU YA FENERBAHCE YA UTURUKI




📌NA MWANDISHI WETU/MTANDAO

MSHAMBULIAJI na nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta amejiunga na klabu ya Uturuki Fenerbahce kwa mkataba wa miaka minne kutoka Aston Villa.

Klabu hiyo imeandika katika mtandao wake kwamba imemuongeza nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania katika kikosi chake kwa mkataba wa miaka minne.

Mbwana Samatta aliyeshinda taji la mfungaji bora mara kadhaa nchini Ubelgiji kabla ya kujiunga na Aston Villa nchini Uingereza atahudumu katika klabu hiyo kwa mkopo wa mwaka mmoja kabla ya kuandikisha kandarasi ya kudumu ya miaka minne.

Mshambuliaji huyo amecheza michezo 14 ya Ligi Kuu ya Uingereza na kufunga goli moja tangu alipojiunga na Aston Villa mwezi Januari 2020.


Samatta pia meichezea Aston Villa michezo miwili ya Kombe la Ligi (Carabao Cup) na kufunga goli moja dhidi ya Manchester City katika mchezo wa fainali wa kombe hilo ambako City walishinda kwa ushindi wa 2-1.


Post a Comment

0 Comments