SERIKALI YAJIVUNIA MATUNDA MIFUMO YA UKUSANYAJI MAPATO KIELEKTRONIKI



 ðŸ“ŒNA FAUSTINE GALAFONI

SERIKALI imesema kuwa makusanyo ya fedha yameongezeka kutoka Bilioni 688.7 kwa mwaka wa fedha 2015/2016 hadi kufikia trilioni2 na bilioni 699 kwa mwaka wa fedha 2019/2020 hiyo ni kutokana na kuwepo kwa mifumo ya ukusanyaji maduhuli kwa njia ya kielektroniki.

Hayo yameelezwa leo  Sept 16,2020 Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,Dotto James wakati wa mawasilisho ya utafiti wa GePG inavyotumika katika Taasisi za Serikali uliofanywa na wataalam toka  Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam. 
James amesema kuwa kuwepo kwa matumizi ya mifumo hiyo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa maduhuli katika Taasisi za Serikali imeleta mafanikio makubwa katika uongozi wa Rais Magufuli ikiwa ni pamoja na kusaidia kuondoa mianya ya wizi,kuwepo kwa uwazi  na uwajibikaji kwa watumishi.
Hata hivyo amewataka maafisa masuhuli ambao wanasimamaia miradi yenye misamaha ya kodi kuwasilisha taarifa za  misamaha ya kodi VAT kupitia mifumo hiyo ya kielektoniki.
Awali akiwasilisha utafiti huo  wa matumizi ya mfumo wa malipo ya Serikali kwa njia ya kielektroniki GePG,Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam,Profesa Joel Matebe amesema kuwa utafiti huo  ambao ulikuwa unapima tathmini umefanyika  katika Taasisi za Serikali 306 na Mikoa 11 imeonyesha kuongezeka kwa maduhuli Pamoja na uaminifu huku akiitaka Serikali kuwaondolea changamoto za kiutendaji kwa  watendaji wa mifumo hiyo.
Nao baadhi ya watumiaji wa huduma hizo akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la hifadhi ya jamiiNSSF)William Erio amebainisha mafaniko yaliyopatikana tangu waanze kutumia mfumo huo mwaka 2018huku Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa bima ya Afya nchini NHIF,Alexander Sanga amesema mfumo huo umeongeza uwajibikaji pamoja na uwazi.

GePG ni Mfumo wa kielektroniki unaowezesha ukusanyaji wa fedha za umma kielektroniki ambao umebuniwa na kutengenezwa na wataalamu wa ndani wa Serikali.
Aidha na  upo kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Umma (Public Finance Act, 2001) ya mwaka 2001 kupitia marekebisho ya mwaka 2017 (Sura 348), na Waraka wa HAZINA Namba 3 wa mwaka 2017 huku Mfumo huu ulianza kutumika rasmi mnamo tarehe 01 Julai 2017 ambapo ulianza na taasisi saba (7)Kwa sasa Mfumo huu unatumiwa na taasisi za Umma 668. 


Post a Comment

0 Comments