JWT 'WALIA' NA WACHINA



📌HAMIDA RAMADHANI

JUMUIYA ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) wamelalamikia kitendo cha wafanyabiashara wa Kichina kuingilia  soko kuuza bidhaa zinazouzwa na wazawa

Aidha jumuiya hiyo imesema Wachina hao wanafanya biashara za kichuuzi ambazo zinafanywa  na wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Wamachinga hivyo kufanya mazingira ya Biashara kwa wazawa.

Akizungumza Jijini hapa katika mkutano wa wenyeviti na makatibu wa  jumuiya hiyo Mwenyekiti wa JWT  Silva Kyando alisema kuwa Wachina hao wanafanya mazingira ya Biashara kwa Wamachinga hususani wa Kariakoo kuwa magumu

Unajua Wachina kule  kwao wanapata mikopo yenye riba nafuu kuliko sisi hivyo wakileta.biashara hapa chini Wana uwezo wa kuuza bei ya chini kuliko mfanyabiashara mzawa, hiyo inaua soko la Watanzania.

Silva Kyando

Amesema kuwa Wachina Kule.kwao wanapewa mikopo yenye yenye riba kuanzia asilimia 6 Hadi asilimia 5.5,wakati mikopo inayotolewa hapa nchini ni asilimia 20 hadi 40.

Aidha Kyando amesema kuwa Wachina hao wamekuwa wakilindwa na.Mamlaka husika hata wakipeleka malalamiko yao hayasikilizwi hivyo wanajikutaa wanaishi katika nchi yao Kama watoto Yatima.

Tunawapenda Wachina ni marafiki zetu wa muda mrefu,lakini hatutaki kuingiliwa soko letu ,wao ni wawekezaji siyo kuja kufanya Biashara ambazo Wamachinga.wanafanya. Kyando 

Mbali na hilo Mwenyekiti huyo amesema kuwa kutokana na.mazingira ya kulindwa Wachina.hao wamekuwa wakwepaji Kodi wakubwa kwani Kuna wakati wanashusha makontena hakuna risiti za EFD Wala leseni hivyo wanajikutaa wakiuza kwa faida kubwa.

Mwenyekiti huyo amesema Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John  Magufuli ni sikivu .wanaamini Changamoto ya Wachina itafanyiwa kazi.

Aidha mbali na Changamoto ya Wachina Mwenyekiti huyo amesema tozo ya Service levy ni kero kubwa kwa Wafanyabiashara hivyo wanaomba Serikali ifute kwani wao siyo walengwa.

Kyando pia aliitaka Serikali kutumia hekima  kuwatafutia maeneo maalum ya kufanyia Biashara Wamachinga kuliko kupanga bidhaa za mbele ya maduka.

Unakuta Mmachinga kapanga bidhaa zake mbele ya duka ambalo na lenyewe lina uza bidhaa ileilei hivyo wanawazibia riziki wenye maduka kwani wao wanauza kwa bei ya chini.


Silva Kyando

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa Dkt. Godwin Wanga amesema Serikali ipo pamoja na wafanyabiashara hao, ambapo aliahidi Changamoto hizo zitapelelwa sehemu husika.

Post a Comment

0 Comments