BMT KUWAONDOA VIONGOZI VING'ANG'ANIZI

 

📌Na Ramadhan Hassan

MKURUGENZI wa michezo nchini,Yusuph Singo ameliagiza Baraza la Michezo Nchini (BMT) kuwaondoa madarakani viongozi wa  vyama vya michezo wanaong'ang'ania madaraka bila kufuata Katiba.

Akizungumza leo Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC),Mkurugenzi huyo wa michezo amesema Serikali imeanza kutafsiri kwa vitendo kauli ya Rais,Dkt.John Magufuli ya kutaka sekta ya michezo kuboreshwa.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa vyama vyote vya michezo nchini,pamoja na baadhi ya wanamichezo waliowahi kufanya vizuri na kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Mkurugenzi huyo ameliagiza BMT kuwaondoa viongozi ambao wanaokaa madaraka bila kufuata Katiba.

"Nawaagiza BMT mzaha sasa umepitwa na wakati viongozi hawataki kuondoka muwaondoe,nendeni vizuri,viongozi ambao hamtaki vyama ni kwa niaba ya Watanzania tu.

Tunatarajia kutoka sehemu moja kwenda nyingine Tennis nawapongeza Sana hatutaki kusikia mnalalamikiana

Yusuph Singo.

Pia,amevitaka vyama hivyo kuhakikisha vinaendeleza michezo kama ilani ya uchaguzi ya BMT inavyotaka.

"Sasa Mheshimiwa Rais anasema Watanzania wanataka ushindi,ndugu zangu tuhakikishe tunaendeleza michezo hata ilani ya uchaguzi inalizungumzia hilo.

"Sisi kama Serikali tumeanza kutafsiri maelekeazo ya Rais na nyie viongozi nendeni mkatafsiri mazoea yamekwisha,hamuheshimu hata Katiba zenu,ninaomba kila mmoja wenu mtakaporudi jipangeni,"amesema.

Katika hatua nyingine,amesema Desemba 19 mwaka huu,Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Innocent Bashungwa anatarajia kukutana na wadau wa michezo vikiwemo vyama vya michezo kumzungumzia mpango wa Taifa wa michezo.

Hivyo amevitaka vyama hivyo kupeleka viongozi sahihi na sio kutuma Wawakilishi.

"Hili ni very serious nitakuwa na mkutano Tarehe 19 kutakuwa na mkutano wa wadau tunaongelea mpango wa Taifa wa kuendeleza michezo,nawaomba mje,msitume wawakilishi,"amesema.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments