JAMII INAVYOAMINI KUHUSU SUALA LA USAFI.

 

 


📌 BONIPACE RICHARD.

SUALA la kunawa mikono limekuepo tangu enzi, Nakumbuka ingali wadogo tulikuwa tukihimizwa kunawa mikono kwa maji safi na salama kwa kutumia sabuni ili kujikinga na magonjwa ya milipuko yanayo sababishwa na uchafu hasa unapotoka chooni na pale unapomaliza kula.

Historia hiyo inasadifu kuwa suala la usafi ni sehemu yetu ya maisha kwani tumekuwa tukifundishwa shuleni utaratibu wa kunawa mikono kwa maji safi  na tiririka ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko.

Mtiririko huo unaosadifu kuwa kampeni ya kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni iloianza tangu jadi na kabla ya janga la ugonjwa unaosababishwa na virusi vya CORONA (Covid 19)

Hata hivyo,utamaduni wa kunawa mikono mara kwa mara ni muhimu katika Maisha ya kila siku ya mwanadamu, kwani ni njia sahihi ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko yanayo sababishwa na uchafu ikiwemo kuhara, kichocho kipindupindu nakadhalika.

Magonjwa kama ya kuhara, kipindupindu, kichocho, na mafua yanayosababishwa na virusi vya Corona ugonjwa wa zika na magonjwa mengine ya mlipuko yanasababiswa na uchafu huku njia inayoeneza maambukizi hayo ikitajwa kuwa ni kupitia njia ya hewa pamoja na kugusana.

Aidha,hutegemea hulka ya mtu na mtu katika kuzingatia usafi wake mwenyewe.

Hata hivyo Kuna baadhi ya watu huzembea kwa makusudi kutokunawa Kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni licha ya kuwepo kwa elimu dhidi ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko yanayosababishwa na uchafu.

 JAMII

Kwa Upande wa Jamii hasa wakazi wa mkoa wa Dodoma,kuhusiana na hali ya unawaji mikono katika kuhakikisha wanajikinga na magonjwa yanayosababishwa na uchafu wamesema kwasasa hawana hamasa kama kipindi cha mlipuko wa mafua yanayosababishwa na virusi vya Corona.

“hamasa ya unawaji wa mikono huanzia kwenye familia, shuleni, ofisini na sehemu zote zenye mikusanyiko umepungua”

Akiongea kwaniaba ya wakazi wenzake, Happines Gwimile Mkazi wa Ipagala jijini Dodoma Amesema hamasa ya unawaji wa mikono kwa maji safi na tiririka umepungua kwasababu watanzania wameshaondokana na  hofu ya uwepo wa mafua yanayosababishwa na virusi vya Corona.

"Unajua Sisi watanzania tuko hivi  mtanzania akijengewa hofu ni kweli anaingiwa na hofu kwelikweli lakini mtanzania huyo huyo ukimpa matumaini ya kitu chema na moyo wake unakuwa safi na haru" alisema Happines

 Aidha   kutokana na msimamo wa  Tanzania kuwa Tanzania  haina ungonjwa wa Corona (Covid-19) ndio maana unawaji wa mikono na uvaaji wa barakoa umepungua kutokana na kujengewa dhana ya kutokuwepo kwa ugonjwa huo  hapa nchini hali inayopelekea Watu kuacha Kunawa mikono na kuvaa Barakoa.

Ameongeza hii ni changamoto kwetu na hasa Sisi wazazi na wale utakuta mzazi anaelimu ya kutosha juu ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko yanayo sababishwa na uchafu na ikiwemo kutonawa mikono kwa maji safi na sabuni lakini tumekuwa wazito kuwafundisha watoto wetu umuhimu wa Kunawa mikono mara kwa mara hata baada ya kutoka chooni, amesema Happines

Amesema licha kuwahimiza watoto kuzingatia usafi ikiwemo unawaji wa mikono lakini pia hata shuleni hakuna miundombini ya kuwafanya watoto wawe na utaratibu wa Kunawa mikono Kila na baada ya kutoka kujisaidia.

Anaongeza kuwa, kabla ya mlipuko wa ugonjwa wa Corona hapa Nchini, utaratibu wa kunawa mikono haukuwepo sehemu katika sehemu mbalimbali ikiwemo kwenye taasisi zote za serikali maeneo yenye mkusanyiko na kadhalika.

"Sasa hivi Hali imebadilika hamasa ya kunawa mikono imepungua tofauti na awali na  hata ukijaribu kutembea katika Ofisi za umma na Binafsi, vyuo vya elimu ya juu na shule zote za Msingi na sekondari miundombinu ya Kunawa mikono hakuna,"  

Kwa kuongezea tu, Sehemu nyingine Utakuta miundombinu ya Kunawa mikono au madumu ya maji  yamefunikwa na hakuna maji wala sabuni" aliongezaHappines

 NINI KIFANYIKE

Jambo kubwa la kuzingatia ni elimu ya usafi kutolewa na miundombinu ifanyiwe kazi pamoja na kuboreshwa kwa kutengenezwa upya kwani imebainika hivi karibuni kuwa kila sehemu miundombinu ya maji imeharibika hivyo inatakiwa kutengenezwa upya na kuweka maji ya kutosha ili Watu waendelee na utaratibu wa Kunawa mikono ili kujikinga na maradhi yatokanayo na uchafu.

"Kuna baadhi ya maeneo wananchi wanachangamoto ya maji utakuta sehemu ya upatikanaji wa maji ni shida hivyo katika maeneo hayo serikali na Taasisi ambazo zinahusika na uvunaji wa maji ya mvua wahusishwe katika kuhakikisha wanawatatulia changamoto hiyo ili wakabiliane na  magonjwa ya mlipuko.

"Hamasa ya unawaji umepungua leo hii ukiamua kwenda katika Ofisi za Serikali na binafsi nyingi Utakuta madumu ya maji meupe hakuna maji wala sabuni inatakiwa tuendeleze utamaduni wa unawaji wa mikono kujikinga na magonjwa mengine yanayotokana na uchafu"

 KWA UPANDE WA WANAFUNZI SHULENI

Hapa tunakutana na Ally Shomari Ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Mlimwa iliyopo kata ya Miuji jijini hapa anasema suala la unawaji wa mikono katika shule yao halitiliwi mkazo tofauti na hapo wali.

Anasema kipindi cha Corona, katika shule yao kulikuwepo na miundombinu ya maji pamoja na madumu ya maji ya kutosha katika kila darasa ambapo wanafunzi ilikuwa ni lazima Kunawa kabla na baada ya kuingia darasani.

Aidha tangu tangazo la kwamba Tanzania hakuna corona madumu ya maji shuleni yalidumu kwa muda wa wiki mbili tu baada ya hapo madumu ya maji tulipokuwa tukinawia mikono Kwaajili ya kujikinga na corona yalitolewa.

Mwandishi wa makala hii hakuishia hapo ambapo amejaribu kupitia katika maeneo tofauti tofauti na hapa tunakutana na Mwalimu wa shule ya sekondari ya Mtumba Moreen Shitindi anasema katika Mazingira ya shule yao suala la unawaji wa mikono limepungua tofauti na hapo awali kipindi cha corona.

 Anasema ile Hali ya wanafunzi kuvaa barako, Kunawa mikono hamasa imepungua tofauti na kipindi cha mlipuko kwani hata watoto ukiwaelimisha imekuwa vigumu.

"Sisi kama walimu wa Mtumba tunajitahi kuwasihi wanafunzi Kunawa mikono kuendelea Kunawa mikono lakini muitikio wa wanafunzi kutekeleza jambo hilo umekuwa ni mgumu kutekeleza," alisema Mwalimu

Aliongeza kuwa katika Nchi yetu mungu ametupendelea kwani maombi tuliyoyafanya yametukomboa na janga hili ambapo kwasasa tupo huru na salama na hili janga limepotelea mbali.

Kwa upande wake mwananchi kutoka Wilaya ya Chamwino Ikulu Ismail Mbiga amesema ni sawa tu kutokuwepo kwa miundombinu ya maji katika sehemu zote za mikusanyiko ikiwemo shuleni, ofisini na hata masokonio.

Amesema Mungu amesikia maombi yetu watanzania wote baada  ya kufunga na kuomba kwa muda wa siku Tatu maombi yetu yamefika na yamekubalika na ndio maana hadi leo hii tuko Salama.

Sanjari na hayo, ameongeza kuwa Nchi ya Tanzania bado ni Nchi masikini na endapo ingetokea ugonjwa wa Corona ungeendelea hakika tusingeweza kukabiliana nao kwani hata Nchi kubwa za ulaya zimeshindwa kuzuia janga hilo ambalo ni tishio kwasasa duniani kote.

Anasema janga hilo ni janga kubwa ambapo nchi zenye fedha na ambazo zinajiweza kiuchumi zimeshindwa kukabiliana na ugonjwa huu lakini Tanzania tumefanikiwa na yote ni kutokana na maombiambayo mwenye mungu aliyapokea na kutunusuru na janga hilo hatari.

"Hivi ndugu mwandishi wa habari unadhani kama  kungekuwa na huu ugonjwa wa Corona Covid-19 Sisi Tanzania tungebakia mpaka muda huu kweli hakika nakuapia  tungeteketea wote kama Kuku," amesema Mbiga

                                                                          MWISHO

 

Post a Comment

0 Comments