TAKUKURU YAJA NA MBINU MPYA YA KUSHUGHULIKIA WANANCHI.

 


📌BARNABAS KISENGI.

TAASISI ya kupambana na Rushwa Takukuru wilayani Mpwapwa imeanzisha kliniki tembezi ya Kata kwa Kata wilayani mpwapwa kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto mbalimbali katika Kata na kuzitolea ufumbuzi katika eneo husika 

Akizungumza katika Kata ya mima kijiji cha mima Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Mpwapwa Bi Julieth Mtuy amesema lengo la kuanzisha kliniki tembezi ni kuwafikia wananchi kiurahisi huko waliko ambao hawana uwezo wa kufika wilayani kwa haraka kutoa kero zao. 

"Sisi Kama Taasisi ya Takukuru tumeamua kuanzisha mfumo huu wa kuwafikia wananchi huku waliko kwenye kata na vijiji na tumekuwa tukiwasikiliza kero zao na kuwapatia majibu hapo hapo kwakuwa tunakuwa tukiongozana na wataalam mbalimbali wa halimashauri ya wilaya"amesema Julieth
 Kero na changamoto nyingine tuliyobaini ni fedha ya Tasaf katika kijiji cha mima kuna wananchi ambao wanauhitaji lakini hawajawahi patiwa hivyo nimemwagiza mratibu wa Tasaf wilaya na timu yake wafike haraka katika kijiji cha mima wahakiki vizuri na kutupatia taarifa ofisini. 

Nao baadhi ya wananchi wameipongeza Takukuru kwa kuanzisha kliniki tembezi kwani itawasaidia Sana kutokana na wananchi wangi kutokuwa na uwezo wa kusafiri hadi wilayani kutoa malalamiko yao hivyo kwa sasa wamerahihisishiwa kwa kufikiwa walipo vijijini ambako kumekuwa na kero mbalimbali. 

Kliniki hii tembezi ya TAKUKURU wilaya ya Mpwapwa itazunguka katika Kata zote wilayani hapa ambapo tunaongozana na wataalamu mbalimbali kwa lengo la kujibu kero za wananchi ambazo tunakutana nazo katika Kata na vijiji na tutawafikia wanchi wote wilayani hapa kwa lengo la kuwaboreshea huduma jirani walipo. 

 

Post a Comment

0 Comments