JKT YASITISHA MAFUNZO YA KUNDI LA KUJITOLEA KWA MWAKA 2020-2021.

 ðŸ“ŒRAMADHAN HASSAN.


JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limesitisha  mafunzo ya JKT kundi la kujitolea kwa mwaka 2020-2021.

Hivyo, limewataka vijana  ambao walikuwa bado  hawajaripoti wasiende   kuripoti katika makambi waliyopangiwa mpaka hapo itakapotangazwa tena na wale ambao wamefika warejee nyumbani.

Hayo yameelezwa leo Januari 19 2021 na Kaimu Mkuu wa Utawala JKT,Kanali Hassan Mabena alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari.

Kanali Mabena amesema mafunzo hayo yalikuwa yaanze hivi karibuni katika makambi mbalimbali nchini hivyo wameyasitisha kwa muda mpaka hapo itakapotangazwa.

Amesema kutokana na kusitishwa kwa mafunzo hayo JKT inawataka vijana wote ambao walichaguliwa na kuripoti makambini kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya JKT  ya kujitolea warejee majumbani kwao.

Kanali Mabena amesema na wale ambao walikuwa bado  hawajaripoti wasiende   kuripoti katika makambi waliyopangiwa mpaka hapo itakapotangazwa tena.

Post a Comment

0 Comments