ZAIDI YA WATU MILIONI 100 HUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI-MAMA SAMIA.



📌HAMIDA  RAMADHANI


MAKAMU wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watu milioni 100 mpaka 150 hutumia Lugha ya kiswahili kwa ajili ya mawasiliano  na kuzitaka taasisi binafsi kuendeleza kutumia lugha hiyo.

Ameyasema hayo  Jijini Dodoma wakati  alipokuwa kwenye Maadhimisho ya siku ya kiswahili Kitaifa yaliyoandaliwa na mabaraza ya Tanzania bara (BAKITA) na Tanzania Zanzibar (BAKIZA)huku kauli mbiu ikisema"Bidhalisha Kiswahili kwa maendeleo endelevu ya Tanzania".

Aidha amesema kuwa lugha ya kiswahili imekuwa na matumizi mapana huku ikitumika ndani na nje ya nchi kwa kufundishia kwenye vyuo vikuu vya kimataifa  mbalimbali pamoja na shule za sekondari na msingi .

Amesema kuwa lugha ya kiswahili imekuwa ikisikika kwenye Radio za kimataifa ikiwemo BBC na Radio Amerika huku kiswahili kikitumika kama bidhaaa ya kukuza kiuchumi.

Hata hivyo amesema katika kukuza kiswahili, Awamu hii ya tano kupitia Rais John Magufuli  ameweza kukiwekea mkazo kukitumia kwenye mikutano mbalimbali na hata kukitumia nje ya nchi wawapo kwenye mikutano.

"Hapo awali hakukuwa na msisitizo kwenye mikutano kuongea kiswahili lakini kupitia Rais wetu John Magufuli ameweza kuimarisha ambapo mikutano inaendeshwa kwa lugha ya kiswahili na sio kiingereza kama mwanzoni  "amesema 


"Nawaomba Taasisi binafsi wasikionee haya Kiswahili kukitumia katika ofisi zao,kwani hiyo ni.mojawapo ya kuendeleza matumizi ya lugha yetu ya Kiswahili kwani Taasisi binafsi asilimia kubwa wanaofanya kazi ni Watanzania amabo wanaongea lugha ya Kiswahili,hivyo wasione ubaya kukitumia lugha ya mawasiliano hivyo Baraza la Kiswahili Tanzania BAKITA na lile la  Zanzibar BAKIZA kuongeza wigo wa misamiati inayoeleweka"amesema Samia

Ametolea mfano neno kusimikwa ambalo amesema kwa upande wa Zanzibar ni neno Kali lenye maana tofauti likitamkwa huku Tanzania Bara.

" Nimekuwa nikiingiwa na ukakasi katika kutamka neno la kusimikwa kwa maaskofu, kwani neno hilo kwetu Zanzibar si neno la kutamkwa hadharani", amesema Suluhu.

Aidha Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada za kuendeleza Kiswahili kwa kuandaa kamusi yenye maneno Millioni 50, lakini mpaka Sasa umefikia maneno Millioni 1.5.

Suluhu pia aliwataka Wakurugenzi wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo kutoa fungu kwa kuendeleza lugha ya Kiswahili kwa kuangalia maeneo ambayo Kiswahili hakitumiwi Sana.

Amesema kuwa BAKITA na BAKIZA wapewe Rasimali Watu,Fedha na watalaamu na kutoa machapisho yachapishwe kwa wingi ili yasambazwe sehemu mbalimbali.

Naye Naibu Waziri wa Habari Utamaduni.na Michezo Abdallah Ulega amesema Lugha ya Kiswahili inaenea kwa Kasi, kwani Leo lugha hiyo imekuwa si Mali ya pekee imekuwa ikitumiwa nchi nyingi Duniani.

" Hivi Sasa Duniani Kiswahili no bidhaa ambayo, Watangazaji,waandishi wa habari, watafsiri Wana soko kubwa la kupata kazi"' amesema Ulega.

Katika maadhimisho hayo Makamu wa Rais amezindua kitabu chenye muongozo wa kufundishia watu kutoka nje

Post a Comment

0 Comments