PINK HIJAB INITIATIVE TRUST YASAIDIA WANAFUNZI 1000 MAHITAJI YA SHULE.


📌HAMIDA RAMADHANI DODOMA

JUMLA ya Wanafunzi 1000 Wilayani Bahi Mkoani Dodoma wamefanikiwa kusaidiwa mahitaji ya shule na Taasisi ya Pink Hijab Initiative Trust iliyopo Jijini hapa.

Akiongea Katika siku ya Maadhimisho ya Hijab Day Kimataifa iliyofanyika Jijini Dodoma Abubakari Khamisi Katibu wa Pink Hijab Tanzania amesema  Pink Hijab inafanya ushirikiano kusaidia jamii kwa maeneo tofauti tofauti nchini.

Amesema kwa  mwaka 2021 walidhamiria kusaidia wanafunzi 1000 na tayari wameshasaidia shule mbili ambazo ni shule ya Bahi Sokoni wanafunzi 100 na shule ya msingi Bahi Misheni wanafunzi 100 mahitaji mbalimbali ya shule.

Kwa Upande wake Aisha Nobe Mwenyekiti wa Wanawake Wilayani Kondoa Bakwata Amewataka Waumini wa Kislam kuelewa na kutambua kwamba  uhamisishaji wa Pink Hijab Sio tu Wavae Hijab kufunika vichwa vyao na badala yake wabadilike kuanzia matendo yao.

Amesema kuvaa Hijab ni wajibu wa Waumini wote wa Kislam hivyo serikali na Taasisi zote mashirika washirikiane ili kutokomeza Hijab zisizokuwa za kisheria na hazina radhi za mwenyezi Mungu. 

Naye Naibu Mwenyekiti wa Shamsia Women and Children Organization Tunu Dachi amewataka wanawake wa Kislam  kuhakikisha wanatuamia vizuri rasilimali Muda kwani akina mama wengi wamekuwa wamejibweteka na kusubiria kuletwa na waumezao.

Amesema Uchumi ni Rasilimali hivyo amewataka akinamama hao kuacha kujitenga na kuhakikisha wanajikite Katika kazi za kujikwamua kiuchumi na kujiingizia fedha.

"Basi tutakapo amka na kuanzisha miradi yetu mbalimbali tuhakikishe tunaugana mikono sio leo kwakuwa fulani kafanikiwa kuanzisha biashara ya kachori Mimi Tunu siende kumuungisha eti tu nitamfaidisha jamani Dini yetu ya Islamic  haitaki hayo mambo," amesema Tunu

Post a Comment

0 Comments