WANANCHI WATAKIWA KUJIUNGA NA CHF ILIYOBORESHWA.

 


📌JASMIN SHEMWEPU.

Serikali imewataka wananchi kujiunga na mfuko wa Afya  ya jamii  CHF  iliyoboresha kwani imekuwa msaada mkubwa kule inakotumika kwa kuwa inarahisisha matibabu kwa jamii ikiwemo kupata  Dawa kwa wakati  mtu anapopata matatizo ya kiafya .

Aidha wakuu wote wa mikoa nchini wametakiwa kuwa wahamasishaji wakubwa kwa wananchi kujiunga na CHF iliyoboresha kwani inasaidia kupunguza gharama za afya  kwa kusogeza huduma bora ikiwemo dawa na vitendanishi  kwenye maeneo yote ya kata,vijiji,mitaa na vitongoji.

Naibu waziri  ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia afya  Dr.Festo Dugange amesema hayo katika hafla ya kukabidhi kadi za CHF iliyoboreshwa ICHF kwa wananchi  wa makundi mbalimbali ikiwemo makundi maalum  kutoka  kaya 361,539, kadi zenye  thamani ya shilingi bilioni 4.6 chini ya wadau  HPSS na shirika la PACT .

Akizungumza katika hafla hiyo mkurugenzi wa huduma za afya ofisi ya Rais TAMISEMI Dr.Ntuli Kapologwe pamoja na kuwapongeza wadau wa maendeleo HPSS na PACT kwa mchango mkubwa katika sekta ya afya kwani  lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025  Bima ya afya inakuwa  ni  kwa  wananchi wote na kuondokana na utegemezi  pamoja na kuwa na vyanzo muhimu vya mapato kuendesha shughuli za afya.

Naye Meneja mradi wa HPSS Tuimarishe Afya  Ally Kebby  ameelezea kufurahishwa kwake na namna CHF iliyoboreshwa inavyozidi kupokelewa na wananchi katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba wataendelea kuunga mkono jitihada za serikali kwa kuzidi kutoa elimu kwa wananchi wa makundi yote.

Upande wake mmoja wa  wanufaika wa mradi huo wa  HPSS Tuimarishe Afya maarufu mradi wa  Kizazi kipya Julie Ezekiel  kutoka Hombolo Makulu, ameshukuru kwa kupata kadi ya CHF iliyoboreshwa na kuwataka wananchi wengine kujiunga na mfuko huo.


Post a Comment

0 Comments