WATAALAM WA AFYA WATOA ELIMU YA MAGONMJWA YA MLIPUKO.


📌STEPHEN NOEL.

WATALAAM wa  afya wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma  wasambaa katika tasisi za serikali  ikiwamo shule za Msingi, sekondari,  kwenye Nyumba za wageni kutoa elimu  dhidi ya magonjwa ya mlipuko kama  kipindu pindu, magonjwa ya matumbo pamoja na  ugonjwa Corona au COVID -19.

 Jopo hilo likiongozwa na mganga mkuu wa wilaya hiyo Dkt Archard Rwezahura amesema wizara Afya  maendeleo ya jamii jinsia,wazee na watoto ina utaratibu wa uelimishaji jamii juu hatua za kuchukua dhidi ya magojwa ya mlipuko yanapo tokea na  wananchi kuchukua tahadhari juu ya magonjwa hayo.

 Amesema lazima wananchi wa wilaya hiyo kuchukua tahadhari  ili kujilinda wao wenyewe na familia zao kwa jaguars kanuni za Afya. 

 Naye afisa Afya wa wilaya Mery Mabagwa amesema wameamua kutoa elimu ikiwa  na lengo ni kuwakumbusha jamii juu ya kanuni za afya kujikinga na magonjwa ya mlipuko ya aina zote ikiwamo korona. 

 Amedai Kama wilaya tayari wameshajipanga kutoa elimu kwa tasisi zote zikiwamo shule vyuo, tasisi za dini na nyumba za  wageni, na kuiomba jamii kuendelea  kuchukua tahadhari na  kufuata maelekezo ya wizara ya afya. 

 Mmoja wa wazee wa jadi wilayani Hapa bwana Hassan Kiwogosa amesema pamoja na watalaam kutoa elimu hiyo ya tahadhari pia serikali iboreshe huduma za jamii ikiwamo upatikanaji wa uhakika wa maji katika mji wa Mpwapwa na upatikanaji wa dawa katika hospitalini na katika vituo vya afya huko vijijini .

  Hata hivyo amesema  jamii ipende kutumia dawa za asili ikiwamo kujifukiza na  dawa zingine ambazo zilitumiwa na wahenga kipindi chao na zikawasaidia. 

 Naye  Magreth Boma Mhudumu Hotelin ameiomba serikali na kusema  pamoja na kupewa elimu njisi ya kujikinga na kununua dawa hizo lakini serikali iweke mkakati wa vipimo Kwa wageni wanao ingia ndani ya wilaya. 

 Mwisho. 

 


Post a Comment

0 Comments