DKT. MAHENGE AWATAKA WAKAZI DODOMA KUCHANGAMKIA FURSA BRELA




 ðŸ“ŒMWANDISHI WETU

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt Bilinith Mahenge amewataka Wakazi wa Mkoa wa Dodoma kuchangamkia elimu inayotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa kuwa ina umuhimu mkubwa katika kujikwamua kiuchumi.

Dkt. Mahenge ameyasema hayo leo Aprili 17, 2021 wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakazi wa Dodoma katika Ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Zimamoto, Jijini Dodoma.



Akizungumza katika ufunguzi huo Dkt. Mahenge amewaeleza washiriki kwamba, ili kuweza kufanikiwa katika biashara ni vyema biashara au kazi husika kuwa imerasimishwa na kutambulika kisheria.

Hatua ya kwanza ya kufanikiwa katika biashara ni kuirasimisha biashara na ikwa inatambulika kwa mujibu wa sheria. BRELA wapo hapa Dodoma kwa siku mbili kwa hiyo hii ni fursa kubwa na adhimu

Dkt. Mahenge.

Naye Msimamizi wa Kanda ya kati na Ofisi ya BRELA mkoani Dodoma, Bw. Gabriel Girangay amesema kwamba licha ya elimu hii kwa wote inayotolewa kwa siku mbili lakini pia ofisi zipo tayari kwa ajili ya kuwa hudumia.

Ofisi ya BRELA mkoani Dodoma ipo tayari kuwahudumia na inafanya maandalizi ya kufika katika Wilaya zote tisa za Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi katika maeno yao kuhusu huduma zetu

Girangay

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge (wa sita kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafuzo ya siku mbili kuhusu huduma zinazotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa Wakazi wa Dodoma

BRELA imeandaa mafunzo ya siku mbili (tarehe 17 na 18/04) ili kuwapa wajasiliamali elimu ya kurasimisha biashara zao ili kuweza kupata fursa za kibiashara.


UMEISOMA HII?👇👇👇

WAZIRI MALIASILI NA UTALII ATENGUA UAMUZI WA DKT.KIGWANGALA,ASEMA ULIKUWA KINYUME NA SHERIA

Post a Comment

0 Comments