WAZIRI MALIASILI NA UTALII ATENGUA UAMUZI WA DKT.KIGWANGALA,ASEMA ULIKUWA KINYUME NA SHERIA


 ðŸ“ŒMWANDISHI WETU

WIZARA ya Maliasili na Utalii imefunga rasmi mzozo  uliodumu kwa miaka miwili juu ya eneo la uwindaji kando ya ziwa Natron ambalo lilihusisha Wizara, wilaya ya Longido na kampuni za uwindaji zinazofanya kazi katika eneo hilo, ambao ulionekana  kudhoofisha sekta ya uwindanji na utalii kwa muda mrefu.

Akizungumza mjini Dodoma wakati wa kusoma hukumu ya Maombi ya Marejeo(Admistrative Review) iliyowasilishwa na kampuni ya Green Miles Safari Limited (GSML) walimwomba Waziri afutilie mbali uamuzi ambao ulipitishwa na ofisi yake wa kufuta leseni ya kitalu cha uwindaji cha Ziwa Natron Mashariki kinachomilikiwa na kampuni hiyo.

Dk Ndumbaro amesema kuwa baada ya kupitia na kuzingatia kwa ushahidi  wa pande zote zinazokinzana kwenye mgogoro huo, ameamua kutengua uamuzi na kuongeza kuwa uamuzi huo ulikuwa batili hivyo GSML watakuwa na haki ya kuendesha shughuli zao katika kitalu hicho.
 

Mzozo huo ulishika kasi mnamo Agosti 7,2019,Waziri wa Maliasili na Utalii wa wakati huo Dk Hamis Kigwangala aliandika barua kwa kampuni hiyo kuwataka kusitisha shughuli zao katika kitalu hicho, Dkt Ndumbaro amesema barua hiyo ilikuwa ni kinyume na matakwa ya Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Namba 5 ya 2019 kwa vile haikuonesha kosa la kampuni hiyo.

Barua kutoka kwa Waziri Dkt.Kigwangala kwenda GMSL, (kumb CBA.177 / 389/01/281) ya tarehe 7 Agosti 2019 haikuonyesha sababu yoyote ya kuhalalisha uamuzi wake wa kufuta umiliki wa kitalu hicho, uamuzi huo unapingana na kifungu cha 38 (12) cha sheria hiyo 

Dkt. Ndumbaro

Sehemu hiyo ya sheria inaelekeza kwamba Waziri anaweza, wakati wowote kabla ya kumalizika kwa kipindi cha uwindaji, kufuta leseni ya kitalu cha  uwindaji ikiwa kuna ushahidi wa kutosha kwamba mmiliki ameshindwa kulipa kodi au kutoa taarifa za uongo wakati wa mchakato wa ugawaji wa kitalu hicho.

Sehemu hiyo pia inatoa mwongozo kwa waziri anapaswa kufuta leseni ikiwa mmiliki wa leseni amehukumiwa kwa moja ya  kosa lililopo chini ya Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori, ameshindwa kulipa ada zinazohitajika au deni lingine lolote na eneo lake la uwindaji.

Mbele yangu sina Ushahidi unaonesha kuwa kabla ya kufutiwa umilikiwa kitalu cha uwindaji Muomba Mapitio (GSML) alijulishwa kosa lake na kupewa sababu za uamuzi kama ambavyo kifungu cha sheria kinataka.

Dkt.Ndumbaro.

 Waziri Ndumbaro amebainisha kuwa Barua ya aliyoiandika Waziri (Dkt.Kigwangala)  kwa GMSL inaelezea mamlaka yake katika kufuta umiliki wa Kitalu lakini hailezei kosa ambalo Muomba Mapitio amelitenda kiasi cha kustahili matumizi ya mamlaka ya Waziri na adhabu aliyopewa.

Walakini, Dk Ndumbaro amesema mbali ya sababu iliyotajwa hapo juu, uamuzi wa Waziri wa wakati huo pia haujatoa  fursa kwa GSML kusikilizwa kabla ya kufukuzwa katika kitalu hicho , Dkt.Ndumbaro amesema hiyo  inapingana na kanuni ya haki ya asili (Nature Justice) kama inavyoonyeshwa katika Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori, Sehemu 38 (13).

Uamuzi wa kubatilisha umiliki wa GMSL katika kitalu hicho haukufuata mahitaji ya kisheria na kanuni za utawala bora.

 Dkt. Ndumbaro.



Mkurugenzi wa Green Miles Safari Awadh Abdallah akitoa ushahidi wake katika kikao
kilichofanyika mwezi Machi jijini Dodoma

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa GSML, mshauri wa kampuni hiyo Salim Balleith alitoa shukrani zake za dhati kwa Serikali  kwa uamuzi huo ambao unawapa haki ya kufanya kazi katika kuzuia hadi 2022.

GSML imesema haitochukua hatua  zaidi kama vile kudai fidia kutokana na uharibifu wa mali katika kambi zao za uwindaji ndani ya eneo hilo

GSML haitachukua hatua zaidi dhidi ya Wizara kwa kile kilichotokea. Sisi ni watanzania wazalendo, tulichotaka ni haki yetu tu ya kufanya biashara hiyo katika eneo hilo.

Salim Balieth

                             ANGALIA VIDEO👇👇👇


 UMEISOMA HII?👇👇👇

AFISA WA TAKUKURU AKAMATWA KWA KUOMBA RUSHWA

Post a Comment

0 Comments