WAKULIMA KATA TATU WANUFAIKA NA MRADI WA KILIMO CHA KITUO CHA UTAFITI TARI

 


📌FAUSTINE GIMU GALAFONI.

KATIKA kuhakikisha sekta ya kilimo inaendelea kukua hapa nchini,zaidi ya wakulima elfu 50  kutoka kata 3   Mkoani Dodoma wamenufaika na   mafunzo ya mradi wa kilimo cha mazao yanayohimili ukame ikiwemo mtama,uwele na ulezi chini ya chini ya Taasisi ya Utafiti wa kilimo nchini[TARI]kituo cha Hombolo.

Akizungumza katika siku maalum iliyotengwa kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo mahsusi kwa wakulima ,mratibu idara ya utafiti na ubunifu kituo cha utafiti wa kilimo[TARI] Hombolo  Dkt.Eliud Kongola  amesema wanatoa huduma za utafiti kwa mazao yanayovumilia ukame hususan Mtama,Uwele na Ulezi ambapo ni zaidi ya wakulima elfu 50 wanapata huduma za  ugani kwa kata tatu  za Hombolo Bwawani,Hombolo Makulu pamoja na Ipala katika jiji la Dodoma.

“Kituo chetu kinahudumia wakulima wanaolima yanayovumilia ukame ikiwemo ,uwele,mtama na ulezi hivyo tumekuwa  tukishirikiana halmashauri ya jiji la  Dodoma tuna zaidi ya wakulima 50,000 wananufaika na mashamba darasa haya hususan kutoka kata 3 zinazozunguka  kituo cha utafiti wa kilimo[TARI]Hombolo”amesema.

Mratibu wa   uaushaji  wa Teknolojia   kituo cha utafiti wa kilimo [TARI]  Hombolo Erinesa Sanga  amesema  shamba darasa linamfanya mkulima aelewe zaidi huku Diwani wa Hombolo Makulu Kamishna Gidion Kana akiipongeza TARI kwa utafiti huo kwa vitendo.

Nao baadhi ya Wakulima wameelezea jinsi walivyonufaika na mafunzo hayo ya kilimo cha kisasa ikiwa ni pamoja na kuvuna mazao maradufu zaidi ikilinganishwa na hapo awali.

“Mwanzoni nilikuwa navuna magunia matatu kwa hekta moja lakini baada ya kujifunza kilimo hiki cha kisasa kupitia mashamba darasa nimeanza kuvuna kiasi cha magunia kuanzia 10 na zaidi ,imekuwa faraja kubwa”amesema mmoja wa wakulima.

Post a Comment

0 Comments