POLISI YASHIKILIA WAWILI KWA TUHUMA ZA MAUAJI KUTUMIA GOBOLE

 


 

📌RHODA SIMBA

JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma  limefanya msako wa kukamata wahalifu wa makosa mbalimbali ambapo linawashikilia watuhumiwa wawili waliohusika na mauaji  pamoja  na silaha mbili aina ya gobole zilizotumika katika mauaji hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini hapa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema kuwa tukio hilo la mauaji limetokea katika kijiji cha Nhinhi Wilaya ya Chamwino ambapo watuhumiwa wawili Saimon Kikoti(36) na mwenzake George Mhando (44) walihusika na mauaji ya kumuua Samsoni Kikoti (56) kwa kutumia silaha aina ya Gobole majira ya saa  moja usiku.

Aidha amesema kuwa baada ya kuhojiwa kwa watuhumiwa hao wamekiri kuhusika na katika mauaji kwa kutumia Silaha huku ikielezwa chanzo na sababu kujichukulia sheria mkononi kwa kumtuhumu Marehemu kuwa ni mwizi wa mifugo kwa muda mrefu.

Niwasihi watu muache kujichukulia sheria mkononi kama mtu anatuhumiwa kwa makosa ya uhalifu mtoe taarifa katika kituo cha polisi ili waweze kukamatwa na kufanyiwa uchunguzi dhidi ya makosa yao

Kamanda Muroto.

Muroto amesema katika msako mwingine jeshi la polisi limewakata jumla ya watu 23 wakicheza kamali kinyume na sheria katika mitaa ya Bahi road na Makulu Tarafa na Wilaya ya Jiji la Dodoma .

 Katika msako wa Tarehe 25 mwaka huu mtaa wa Amani kata ya Chang’ombe walikamatwa Maulid Shaka (33)mkazi wa chang’ombe na wenzake 6 wakijuhusisha na vitendo vya uhalifu wa uporaji kwa kutumia usafiri wa pikipiki tofauti.

RPC Muroto akimtambulisha
mmoja wa watuhumiwa.

‘’Watuhumiwa walikuwa wanatafutwa kwa makosa haya mbinu wanayotumia kupakia abiria nyakati za usiku na wengine wanawafuata nyuma na kuwavamia huku wakiwapora wakati abiria anashushwa au akiwa njiani ‘’amesema

‘’Wakati tukiendelea na msako kila sehemu tulifanikiwa kukamata Pikipiki mbili ambazo wamekuwa wakizitumia kufanyia uhalifu huo ambazo ni MC.601 BQL HAOJUE na MCL.154 CJJ BOXER  ‘’amesema Muroto.

Katika hatua nyingine amesema Jeshi hilo lilikamata watuhumiwa mbalimbali waliojihusisha na vitendo vya madawa ya kulevya  Gramu 2.8 ,bangi Gramu 15.4,na pombe haramu ya moshi inayojulikana kama Gongo lita 35 .

Ametoa wito kwa wale wote wanaojihusisha na kumiliki silaha kinyume na taratibu ,wauzaji na wasafirishaji wa madawa ya kulevya ,wanaopokea na kuhifadhi mali za wizi wajilasilimishe wenyewe huku akidai watakao kaidi agizo hilo hawatapona kwenye msako mkali  unaoendelea.

 

Post a Comment

0 Comments