UTALII WA NDANI NI SEHEMU YA LISHE YA AKILI,ILISHE AKILI YAKO MAMBO MAPYA.



📌HAMIDA RAMADHANI

WATANZANIA wametakiwa kuwa na utaratibu wa kwenda kutembelea vivutio vya ndani na kuachana na tabia ya kuona kwamba watu kutoka mataifa ya nchi nyingine ndio wanastahili kuja na kufanya utalii katika hifadhi ambazo ni tunu za watanzania.

Dhana hii imejengeka katika vichwa vya watanzania kwa muda mrefu hali inayopelekea hadi kizazi cha sasa kuona hakuna umuhimu wa kwenda kufanya utalii.

Tunapo zungumzia Utalii ni kile kitendo cha kusafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa lengo la burudani,biashara kujifunza au makusudi mengine.

Kufuatia suala la utalii wa ndani kuendelea kuzorota katika nchi nyingi za Afrika,baadhi ya asasi binafsi na makampuni ya utalii Tanzania,yameanza kutafuta mikakati ambayo itasaidia kuamsha ari ya raia kutembelea vivutio vyao na kuachana na dhana kudhani kuwa utalii ni kwaajili ya wanaotoka nchi za Ulaya tu.

Kwa miaka mingi tumekuwa hatuna utaratibu wa kutembelea vivutio kwenye maeneo mbali mbali kama vile hifadhi, sehemu za kihistoria, makumbusho, na sehemu nyingine zinazovutia.

Mara nyingi watu wengi wanaposikia masuala ya utalii, huwa wanajitoa kabisa na kuona kuwa hawastahili kuwa kwenye kundi la watalii, wanaamini watalii ni wazungu tu.

Wengine wanafanya hivyo kwa kuwa hawajaona faida za kuwa watalii, hawaoni faida za kutembelea maeneo yenye vivutio mbali mbali hapa nchini.

FAIDA



LISHE YA AKILI

Unaposafiri kwa lengo la kwenda kuona wanyamapori au vivutio vingine mbalimbali ambavyo hajawahi kuviona huwa akili yako inafurahi na kuwa kama mpya, unaipa akili yako chakula, kama tunavyojua kazi ya akili zetu ni kufikiri, na huwezi kufikiri kitu ambacho hujakiona au kukisikia au hata kukisoma, kwa hiyo unapo kuwa mtalii, maana yake unailisha akili yako mambo mapya, ambayo utayatafakari.

Naweza kusema kama vile unavyosoma kitabu na kufurahia mambo ambayo ni mageni kwako, je si zaidi kuyaona mambo mageni kwa kutembelea hifadhi mbali mbali, au sehemu mbali mbali zenye vivutio? Ilishe akili yako mambo mapya.

MARAFIKI

Naamini ukikutana na watu wapya kwenye maisha yako, hata mambo mapya yanaanza kuingia kwenye maisha yako, kama una marafiki wa muda mrefu na hujawahi hata kuwa na marafiki wengine tofauti na hao wa miaka mingi, hii ni fursa yako ya kukutana na watu wapya.

Watu ndio wanamchango mkubwa kwenye mafanikio na ndoto zako, jipatie watu sahihi kila uwezapo kwenye maisha yako, watu ni fursa watu wana vitu vizuri Hivyo unaweza kukuza mtandao wako na watu wengine kwa upya kabisa Wanasemaga tembea uone.

ELIMU

Unapotembelea hifadhi au maeneo yaliyohifadhiwa, unapata nafasi ya kuelimika na kupata maarifa kwa njia mbali mbali kama kwa kuona mwenyewe na pia kwa njia ya kufundishwa na kuelekezwa na wataalamu walioko maeneo hayo Kwa kupitia maelezo na taarifa utakazopata itakusaidia kujifunza vitu mbali mbali vitakavyo saidia kuboresha maisha yako na uhifadhi wa maliasili zetu.

Pia kama ni wanafunzi au ni watoto wataelewa misingi na wataweza kuchagua kuingia kwenye fani ya kusomea mambo ya wanyamapori na utalii, wengine itawasaidia na kuwapa maeneo ya kufanya tafiti mbali mbali za kisayansi na za kijamii.

KUINUA UCHUMI NA KUHARAKISHA MAENDELEO.


Watu wanapokuwa na utamaduni wa kutembelea hifadhi na maliasili nyingine wanakuwa ndio wachangiaji wakuu wa ukuaji wa uchumi wetu kwa kuongeza mapato ya ndani Kupitia utalii na maliasili.

Kwa kiingilio ambacho watatoa kwenda hifadhini au maeneo ya vivutio itasaidia sana kuinua uchumi wa nchi yetu ni njia nzuri sana ya kuanzia ili tuitoe nchi yetu kwenye utegemezi mkubwa wa misaada ya kifedha kutoka kwa mataifa mengine tukiwa na utamaduni wa namna hii wa kutembelea hifadhi na vivutio mara kwa mara, tutaipeleka nchi yetu mbali  kiuchumi.

Naamini umepata mwanga na sababu za msingi kabisa za kutembelea maeneo ya vivutio, kuna sababu nyingi lakini hizo saba zitufikirishe Usisahau kumshirikisha mwingine makala hii. Jijengee utaratibu huu, ni mzuri sana utaimarisha afya ya akili na afya ya mwili na roho yako pia.

Hapa tunakutana na Shirika la hifadhi za taifa TANAPA ambapo shirika hili limepewa dhamana ya kusimamia ,kuendeleza maeneo yalioanzishwa kisheria kuwa hifadhi za taifa .

Maeneo hayo yanawakilisha kiwango cha juu kabisa cha uhifadhi wa wanyama pori, ambapo kwa wakati huu shirika linasimamia hifadhi 22 eneo linalosimamiwa na hifadhi ya taifa ni takribani kilometa za mraba 404,464 sawa na asilimia 11 ya eneo.

 

MADHUMUNI

Madhumuni ya Shirika la uhifadhi Tanzania TANAPA ni kuhifadhi maeneo yaliyo na thamani/sifa za kipekee zinazoonesha urithi wa mali za kiutamaduni au maliasili za taifa .

Paia kuhifadhi maeneo yenye mifumo bayana ya aina maalumu za maliasili na kuhifadhi vyanzo vya maji na ardhi ambavyo ni muhimu katika kudumisha uwianao na kiikolojia na ambayo vinachangia mahitaji ya kujikimu ya watu waishio karibu na mipaka ya hifadhi na taifa kwa ujumla.

Madhumuni mengine ni kuhifadhi maeneo yanayotoa fursa kwa umma kwa ajili ya manufaa yao kimaisha,kiburudani na taiti za kisayansi.

Hapa tunamuona Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Dodoma Ahamed Mbugi kutoka  TANAPA  amewataka wanahabari  kutumia kalamu zao katika kutangaza utalii wa ndani.

“Kumekuwepo na tabia ya jamii kuamini kuwa kutalii ni mpaka lazima utoke nje ya nchi wakati kuna maeneo mengi ya kufanya utalii ndani ya nchi ambayo hawayafahamu wala kuyatembelea,”

Na kuongeza kusema kuwa “lazima tujenge utamaduni wa kutembelea vivutio vyetu vya ndani zipo nchi ambazo watalii wengi ni wakazi wan chi husika  mfano nchi ya Afrika kusini watalii wengi ni wakazi wan chi hiyo na wamekuwa wakienda muda wote  kutembelea hifadhi na maeneo mbalimbali ya kitalii katika nchi yao,” amesema Kamishina Mbugi.

Pascal Shelutete ni kamishina uhifadhi msaidizi mwandamizi wa mawalisiano wa TANAPA anaeleza kwamba  kwasababu watanzania jamii muamko bado ni mdogo wameanda mpango mkakati wakuboresha na kuendelea kutangaz vivutio vya kitalii kupitia Televisheni ikiwemo Tanzania safari Channel,Channel ya shirika la utangazaji Tanzania TBC ,vipindi vya radio na mitandao ya kijamii.

Anabainisha shirika linatoa fursa kwa sekta binafsi katika kuendeleza na kukuiza utalii katika hifadhi za taifa kwa kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi na umma ili kuwekeza katika meneo ya hifadhi.

Nae  Ofisa uhifadhi Mkuu wa shirika hilo July Lyimo amesema utalii husaidia kukuza uchumi na pato la taifa,kuongeza ajira , nakuitambulisha nchi kwa ujumla.

“Niwaombe waandishi wa habari mtumie kalamu zenu katika kuhakikisha tunawaelimisha ,hamasisha watanzania kuona umuhimu wa kwenda kutembelea Hifadhi za Taifa,”amesema July

 


Post a Comment

0 Comments