MWENYEKITI JUMUIYA YA MARIDHIANO DODOMA AWASIHI VIONGOZI WA DINI KUHUBIRI AMANI NA KUEPUKA UBAGUZI WA KIDINI


 

Na Josephine Mtweve, Zainabu Mtoi na Agness Peter,

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Maridhiano Mkoa wa Dodoma, Mch.Evance Chande amewataka viongozi wa dini kuhubiri amani na kuepuka ubaguzi wa kidini 

Akizungumza na waandishi wa habari katika ibada ya kuombea miradi mbalimbali katika sekta ya elimu, afya, miundombinu na sekta nyingine, Mch.Evance amesema miradi hiyo imewekwa wazi maalumu kwaajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi.

Amesema lengo la Serikali ni kuboresha miundombinu katika sekta mbalimbali ili kuwasaidia wananchi kupata huduma za kijamii pamoja na maendeleo ya nchi.

"Maendeleo kama uwanja wa ndege, na shughuli nyingine kama ujenzi wa maghorofa ya Wizara katika mji wa Serikali hizo zote zinahitaji kuwekwa mbele za Mungu, Mungu aonekane awasaidie watendaji watakaochukua nafasi ya kufanya mambo hayo yote tuwaombee kazi ifanikuwe,"alisema.

Aidha amesema kazi ya watanzania ni kuwaombea viongozi wao wa nchi ili waendelee kuongoza nchi na kuleta maendeleo pamoja na kulinda amani ya nchi yao.

"Amani ndio kila kitu kwahiyo watanzania tusikubali kumwacha mtu aharibu amani ya nchi hata kama amesema sana,"aliongeza

Kwa upande wake mmoja wa waumini wa kanisa hilo, Joyce Evans amesema miradi hiyo itawanufaisha wajasiriamali wadogo wadogo akitolea mfano wa mama lishe kuuza chakula kwa wajenzi wa miradi hiyo.

Aidha amewaomba wasimamizi wa miradi hiyo kuwa wazalendo, waaminifu kwaajili ya nchi na Rais kwani kwa kufanya hivyo kutazaana maendeleo na mafanikio.

Post a Comment

0 Comments