WAZIRI MWAMBE AWATAKA WATANZANIA KUDUMISHA AMANI ILI KUVUTIA WAWEKEZAJI

                                                       


 

Na, Sophia Mohamed, Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwekezaji Mhe. Goffrey Mwambe amewataka watanzania kudumisha amani na utulivu ili kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza Nchini Tanzania.

Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari Jijini Dodoma  katika mwendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara Waziri Mwambe amesema, njia mojawapo ya kuvutia wawekezaji ni watanzania kudumisha amani na utulivu ili wawekezaji wajue wanakuja kuwekeza sehemu salama.

“Watanzania lazima mudumishe amani na utulivu ili wawekezaji kutoka nchi mbali mbali waweze kuja kwa wingi kuwekeza hapa nchi Tanzania.” Amesema Waziri Mwambe.

                                              


Aidha Waziri Mwambe amewataka watanzania kuthubutu  wenyewe kuwekeza katika Sekta zilizopo hapa nchini,kutoa ushirikiano na kuunga mkono Serikali ya awamu ya sita ili kuendeleza uchumi wa Tanzania.

“Watanzania mnatakiwa kushiriki katika shughuli mbali mbali za kiuchumi ili kuweza kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Tanzania inakuwa kichumi.”amesema Mwambe

Mbali na hayo Mwambe amewaeleza watanzania kutumia rasilimali zilizopo nchini kama vile bahari ili  kujiletea maendeleo yao binafsi na nchi kwa ujumla.

                                                    


Hata hivyo Waziri Mwambe amesema kumekuwepo na mabadiliko ya kikodi na yale yasiyo ya kikodi kwa kuondolewa kwa kodi ambazo si za lazima zaidi ya 236,pia wamefanya maboresho mbali mbali ya sheria  ya uratibu wa ajira za wageni ili kuwaraisishia wawekezaji kuwekeza nchini bila usumbufu wowote.

“Tumefanya maboresho ya sheria  ya uratibu wa ajira kwa wageni ili kuwahamasisha wawekezaji kuwekeza nchini Tanzania, pia tumeboresha vibali vya waamihaji ili kuraisisha uwekezaji kuwa mkubwa hapa nchini.”ameasema Waziri Mwambe

Waziri Mwambe ameongeza kuwa dhamira ya Raisi Samia ni kutaka ukuaji wa uchumi kufiikia asilimia 8 ambayo itawezesha kuimarisha  uchumi imara na kuzalisha ajira zaidi.

  

 

Post a Comment

1 Comments

  1. The King Casino | Review of Casino | RTP - Joker
    The king https://jancasino.com/review/merit-casino/ casino septcasino review 토토 - everything you 바카라 사이트 need to know about this popular worrione casino. It's all about quality and quantity.

    ReplyDelete