WANANCHI WAASWA KUNUNUA DAWA KWA MAELEKEZO YA WATAALAMU WA AFYA

 


📌RHODA SIMBA

MSAJILI wa Baraza la Famasia nchini  Elizabeth  Shekalaghe amewataka wananchi  kuacha kujichukulia maamuzi ya kutumia au  kujinunulia  dawa kiholela bila maelekezo ya wataalamu wa afya kuwa wapo katika hatari  ya kupata usugu wa vimelea.

Aidha amesema pia kutotumia dawa kwa usahihi pia kunaweza kusababisha vifo, maradhi ya figo na ini na usugu wa vimelea katika ugonjwa.

Ameyasema hayo  leo Disemba 10 jijini hapa  wakati akizungumza na waandishi wa habari  ambapo amesema   kumekuwa na mazoea ,ya wananchi  kujichukulia dawa bila usahihi pasipo kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.

“Ni vyema wananchi mkafahamu kuwa zipo athali za matumizi yasiyo sahihi ya dawa ikiwemokuongezeka kwa ugonjwa, kutopata nafuu,kutopona na hatimaye kupelea kifo,matumizi ambayo huongeza gharama za matibabu,kuongezeka kwa madhara  na usugu wa vimelea vya magonjwa  katika dawa na kusababisha maradhi ya figo na ini,”amesema

Amesema zipo faida zitokanazo na matumizi sahihi ya dawa ikiwemo kupunguza uwezekano wa kujenga usugu wa vimelea , kupunguza maradhi yatokanayo na usugu wa vimelea vya magonjwa.

Ametaja faida nyingine kuwa ni kupunguza uwezekano wa kupata  magonjwa yatokanayo na utumiaji usugu wa dawa , kuboresha af ya mtumiaji wa dawa hivyo kupona kwa wakati pamoja na kjenga imani na mifumo ya kutolea huduma za afya.

 Katika hatua nyingine msajili huyo amewataka wafamasia wote nchini kuakikisha wanauhishwa leseni zao kabla ya 30 Disemba mwaka huu kupitia mfumo wa kielekroniki ili   ili kurahisha utendaji.

Kuhusu udhibiti wa maduka ya famasi Msajili huyo amesema mkakati ikiwemo kuendelea na ukaguzi wa kila siku wa kukagua ili kubaini wanaokiuka na sheria kuchukua mkondo wake.

Natoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanapata dawa katika maeneo ambayo yamesajiliwa na kwa duka la dawa ambalo litatoadawa bila cheti cha daktari  adhabu yake ni faini isiyopungua milioni tano au kifungo cha miezi 12

Shekalaghe amewataka wamiliki wa famasi wanaoongeza marembo au kuweka matangazo ili kuvutia wateja kuacha mara moja kwani ni kinyume na kanuni za afya

“Niwaombe sana wamiliki wa maduka ya famasi kuacha mara moja na endapo tutakuta kuna ukiukaji wa sheria au kanuni tumeelekezwa kufunga famasi hiyo,”amesema

 

Post a Comment

0 Comments