EWURA:BEI YA MAFUTA YA TAA ITATEGEMEA GHARAMA ZA USAFIRISHAJI KUTOKA DSM




📌RHODA SIMBA

 

MAMLAKA ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya ya mafuta ya petrol dizeli na mafuta ya taa yaliyopokelewa bandari ya Dar es Salaam huku Petroli na Mafuta ya taa yakishuka bei na dizeli kupanda.

 

Hayo yamesemwa hii leo jijini hapa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Godfrey Chibulunje wakati akitangaza bei mpya itakayoanza kutumika hapo kesho februari 2 ambapo  amesema mafuta ya petrol yamepungua kwa shilingi 21 kwa lita, mafuta taa  shilingi 44 kwa lita na dizeli imepanda kwa shilingi 13 kwa lita.

 

Bei za rejareja kwa mafuta ya petrol na dizeli kwa mikoa ya kaskazini, Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara  zimepungua kwa shilingi  123 kwa lita petro na shilingi 92 kwa lita kwa dizeli mtawalia

“Kutokana na kumalizika kwa mafuta ya taa kwenye maghala ya  kuhifadhia yaliyopo Tanga  waendeshaji wa vituo vya mafuta katika kanda ya kaskazini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka katika bandari ya dar es salaam na hivyo bei za rejareja  katika mitaa hiyo itakuwa kulingana na gharama za kupokelea” amesema Chibulunje.

 

Amesema bei za reja reja za mafuta ya petrol na dizeli kwa mikoa ya kusini Mtwara Lindi na Ruvuma zitaendelea zile zile zilizotangazwa katika toleo la tarehe 05 january 2022 hii ni kwasababu kwa mwezi January hakuna shehena ya mafuta iliyopokelewa kupitia bandari ya Mtwara.

 

Pia kwa kuwa hakuna maghala ya kuhifadhi mafuta ya taa katika bandari ya Mtwara waendeshaji wa mafuta wa mikoa ya kusini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka katika bandari ya Dar es salaam na hivyo bei za reja reja  za mafuta ya taa katika mikoa hiyo itakuwa kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya taa kwa kutumia bandari ya Dar es salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika

  

Post a Comment

0 Comments