NAPE AWATAKA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA HABARI KUFANYA KAZI KWA BIDII NA WELEDI

 


 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

WAZIRI wa Habari  Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amewataka wafanyakazi  Wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa  bidii na weledi kwa kuzingatia misingi ya sheria haki na ustawi kwa wateja wanaowahudumia.

Waziri Nape ameyasema hayo leo Aprili 30 jijini hapa  katika kikao cha wafanyakazi na Serikali na afya TUGHE  ambapo amesema  baadhi ya watumishi wa umma  wanafanya kazi kwa mazoea hali  inayoathiri uwajibikaji wa pamoja katika utoaji wa huduma  kwa  wananchi.

“Ninawaomba Watumishi tuache kufanya kazi kwa mazoea, ondokeni katika kufanya kazi kwa analojia na badala yake tuhakikishe tunafanya kazi zitakazoacha alama,

“ Kila binadamu ana vipawa ambavyo Mungu amempa, ni matumaini yangu kwamba haya tunayoanza kuyajenga sisi wafanyakazi tutayatumia vizuri, tutimize wajibu wetu na kila mmoja kwenye eneo lake aone umuhimu wa kuwa hapo alipo.”amesema Nape

Amesema Wizara hiyo inasimamia miradi mikubwa kadhaa ambayo itabadilisha na ni vizuri kama Wizara wakawa na uelewa wa pamoja wa miradi  kupitia semina mbalimbali.

“Dunia inabadilika na sisi tuko kwenye Wizara ambayo inajenga kesho, mabadiliko ya sayansi na teknolojia, yanabadilisha namna ambavyo tunapaswa kufanya kazi hivyo ni muhimu kila mmoja kwenye eneo lake kuhakikisha anafkiria zaidi ya ‘google’ ili kuonesha umuhimu wa kuwa katika nafasi hiyo”amesema

Nae Katibu Mkuu Wizara ya  Habari  mawasiliano  na Teknolojia ya  Habari Dkt Jimmy Yonazi ameahidi kuboresha  mazingira  ya kazi  kwa wafanyakazi.

“Jambo la kufanya kazi kwa furaha kwangu mimi ni kipaumbele, wajibu na nia, kila mmoja anatakiwa kufanya kazi kwa uhuru na kuruhusiwa kufikiri kwa sababu kufikiri kwa uhuru kunaleta ubunifu,

“Katika ulimwengu wa sasa, uchumi wa kidijitali hauna mipaka, vivyo hivyo kwa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari havina mipaka kwa hiyo, tunamshkuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kuunda Wizara hii na kuifanya nchi yetu kuwa moja ya nchi ambazo zina Wizara mahususi katika sekta hizi.”Amesema Yonazi

Amesema Endapo kila mmoja akifanya kazi kwa bidii na akatumika vizuri katika nafasi yake, Wizara hiyo itakuwa ya mfano ambayo kila mtu atatamani kuhamia.

Kwa upande wake muwakilishi wa TUGHE  Laurencia Masigo amesisitiza umuhimu wa  mafunzo kwa  wafanyakazi ili kuendana na  mabadiliko ya kiteknolojia.

“TUGHE inaipongeza Wizara kwa kupata hati safi kwa mwaka huu, tunawapongeza kwa sababu huo ni mchakato mrefu kuanzia kuweka mikakati na kuifuatilia, kupata fedha na kusimamia kazi mpaka kuja kukaguliwa na Wakaguzi na kupata hati safi, hili ni jambo la kujivunia,

 

Post a Comment

0 Comments