NDEJEMBI AZITAKA TAASISI ZA SERIKALI KUIMARISHA UFUATILIAJI NA TATHMINI.

 


📌RHODA SIMBA

NAIBU Waziri  Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Deogratias Ndejembi, amezitaka taasisi za Serikali kuimarisha ufuatiliaji na tathmini, lengo likiwa ni kuboresha utendaji kazi wa taasisi.

Kadhalika  amesema ufuatiliaji na tathmini unasaidia kupata thamani na matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo kwenye  taasisi za Serikali.

Ameyasema hayo jijini hapa wakati akifunga kongamano la kitaifa la ufuatiliaji na tathmini lililoandaliwa na  umoja wa tathimini nchini  (TanEA)

“Michango  na hoja ambazo mmezitoa wakati wa majadiliano kwenye kongamano hili yatasaidia katika kuboresha eneo hili la ufuatiliaji na tathmini na kuwahakikishia kuyafanyia kazi  yaliyoibuliwa kwenye kongamano hili,

"Kwa niaba ya Serikali niwahakikishie hoja na michango mliyoiwasilisha tutaifanyia kazi ipasavyo, Maana nimejulishwa katika hoja hizo kuna mambo mbalimbali ambayo mmeyagusiwa ikiwemo kuyageuza masuala ya ufuatiliaji na tathmini kuwa kada kamili na kuwa na Bodi yake haya yote tunayachukua kwenda kuyafanyia kazi ili kuona tutafanya nini huko mbeleni,"amesema Ndejembi

Aidha Kongamano hilo la kitaifa la ufuatiliaji na tathmini limetoa maazimio kadhaa kwa ajili ya serikali kuyafanyia kazi ikiwamo kutungwa sera ya masuala hayo.

Akisoma  maazimio hayo Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Nolasco Kipanda amesema washiriki wameomba Serikali kuangalia namna ya kuwa na sera ya ufuatiliaji na tathmini ili suala hilo kutoa nguvu ya kisheria.

Kipanda amesema wamehimiza uwepo wa ushirikiano kati ya Serikali na taasisi zake, wadau na kuishauri watoa maamuzi ili kutumia vizuri matokeo ya ufuatiliaji na tathimini.

“Tukitaka kuona matokeo ya ufuatiliaji na tathmini matokeo ya we na evidence based ( yawe na ushahidi), washiriki wamesisitiza kuwa isionekane kuwa ufuatiliaji na tathimini unachukua nafasi ya ukaguzi ila ni vitu ambavyo vinasaidiana katika kuleta ufanisi,”amesema.

Sambamba na hayo amesema kuna haja ya Serikali kutambua na kuimarisha vya kutosha vitengo vya ufuatiliaji na tathmini na kupatikana kwa rasimali watu na fedha za kutosha. 

“Washiriki wamesisitiza haja ya Serikali na sekta binafsi kuendelea kuangalia maeneo yenye changamoto katika masuala ya ufuatiliaji na tathimini ili yaweze kutafutiwa majawabu,”amesema.

 

 

Post a Comment

0 Comments