MAAFISA UHAMIAJI WATAKIWA KUBUNI MBINU ZA KITEKNOLOJIA KUKABILIANA NA UHALIFU.

 ðŸ“ŒSALMA HAROUN

RAIS wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu amewataka maafisa wa uhamiaji nchini kubuni mbinu mbalimbali za kiteknolojia ili kuweza kukabiliana na mbinu mpya za uhalifu zinazojitokeza mara kwa mara.

Ameyasema hayo leo katika ziara ya kufunga mafunzo ya awali ya askari wa Uhamiaji Jijini Tanga ambapo amewataka maafisa wa jeshi la uhamiaji kufanya kazi kwa weledi na kufuata Sheria na taratibu zilizopo nchini.

Rais Samia amesema kwa kufanya hivyo wataweza kuviwezesha vyombo vya usalama kutekeleza vyema majukumu yake ya ulinzi wa Taifa.

Nimesikia kuna baadhi ya maafisa na maskari wasio waaminifu na kuna kesi katika mafaili kwenye fedha zinazotoka za vibali wanazigeuza za kwao na kuweka mifukoni

Amesema katika utafiti mdogo uliofanywa mwaka huu hususani kwenye vituo vya Zanzibar pamoja na Dar-saalam wamegundua upotevu mkubwa wa fedha za viza ambao unafanywa na maafisa wa uhamiaji.

Aidha Rais Samia ameagiza maafisa hao kushughulikiwa ili iwe fundisho kwa wengine na kurudi katika maadili.

 

Post a Comment

0 Comments