WAFUGAJI NCHINI WATAKIWA KUCHANJA MIFUGO YAO

 ðŸ“ŒSAIDA ISSA

MKURUGENZI wa huduma za Mifugo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Hezron Nonga ametoa wito kwa madaktari wa mifugo nchini kuhakikisha wafugaji wanachanja mifugo yao ili kutokomeza magonjwa yanayoshambulia mifugo ikiwemo ugonjwa wa sotoka na kichaa cha mbwa.

Prof. Nonga ametoa wito huo wakati akikabidhi chanjo kwa wataalamu wa mifugo jijini Dodoma zilizotolewa na chama cha madaktari wa mifugo nchini TVA  zitakazotumika kuchanja mifugo zaidi ya elfu sita ambapo amesema suala la chanjo ya mifugo linapaswa kuwa ajenda ili kutokomeza magonjwa ya mifugo kwa asilimia 70 mpaka ifikapo mwaka 2030.

Wenzetu  hawa wa TVA  wametoa hizi chanjo 1100 zenye thamani ya shilingi milioni  tatu na laki tatu kwa mapenzi mema ili kuwawezesha   wenzetu wakazi wa jiji la Dodoma wanakuwa  salama kwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa

Prof. Nonga.

Amesema Tanzania kama nchi nyingine zipo kwenye ukanda wa kitropikali ambazo  zina joto la wastani zinawezesha vimelea  kustawi na kuzaliana kuna mvua na jua  kiasi unyevunyevu unaowezesha vimelea ambavyo vinaweza kusababisha maradhi kwa mifugo kama minyoo fangasi na maradhi mengine.

Amesema Wizara ilichagua magonjwa 13 kama magonjwa ya kipaumbele  ikiwemo ya kichaa cha mbwa  ambapo amesema  mpango wa serikiali ni kutomeza kabisa ugonjwa wa sotoka ya mbuzi na kondoo pamoja na kichaa cha mbwa ambapo mpaka sasa uchanjaji wa mbwa bado  upo chini  kwa asilimia 45.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha madaktari nchini TVA Profesa Esron Karimuribo amesema   wataendelea kushirikiana na serikali kwa kuzalisha chanjo ya mifugo ili kumaliza magonjwa ya mifugo

Tunaanza chanjo kesho kwa jiji la Dodoma pembezoni kidogo katika maeneo ya Nala Mbalawala lakini pia tutakuja kutoa hadi jiji lengo likiwa ni kutokomeza kabisa kichaa cha mbwa

Karimuribo

Naye Profesa Sharadhuli Kimera-Mwakilishi wa chama cha madaktari wa mifugo  jumuiya ya madola  amesema wao kama madtari wameona kuwa ipo  haja ya kuchangia kuboresha chanjo ya kichaa cha mbwa lengo ni mpaka ifikapo mwaka 2030 kuwe na maambukizi  sifuri ya kichaa cha mbwa.

Hizi chanjo 1100 za kichaa cha mbwa na magonjwa ya mapele ngozi tumekabidhi kwa kuwa sisi tunaelewa ni wapi panahitaji nguvu zaidi na shirika la afya za wanayama wameweka lengo la kuondoa kichaa cha mbwa kwa binadamu kwa maambukizi  sifuri. Ugonjwa huu unaathiri kabisa ngozi ya wanyama, kwa dozi hizi itasaidia kutoa motisha kwa wafugaji kwa kujali masilahi ya wafugaji 

Profesa Kimera

Hata hivyo chanjo hiyo imezinduliwa katika tarafa za Nala na Mbalawala ambapo dozi 4000 zitatolewa kwa mbuzi na kondoo ili kuwakinga na ugonjwa wa sotoka.

 

Post a Comment

0 Comments