WAHITIMU CHUO CHA MIPANGO WATAKIWA KUWA CHACHU YA KUJIFUNZA ILI KUONGEZA MAARIFA NA KUBORESHA UTENDAJI WAO WA KAZI.

 ðŸ“ŒMWANDISHI WETU

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Jenifa Omolo amewataka wahitimu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kuendelea kuwa chachu ya kujifunza ili kuongeza maarifa ,ujuzi na ubunifu unaohitajika katika kuboresha utendaji wao wa kazi.

Ameyasema haya leo katika Mahafali ya 36 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dodoma, ambapo amesema kwa wale watakao endelea na masomo ya ngazi ya juu wanapaswa kuendelea kujifunza kwa bidii ili kupata maarifa na ujuzi utakao wawezesha kuhimili mazingira ya ulimwengu wa kisasa wa kazi ya maendeleo ya uchumi ya familia zao na taifa kwa ujumla.

Nawapongeza wahadhiri wa chuo kwa kushiriki katika kuwapa maarifa na ujuzi wahitimu hawa. Nyie ndio mlikuwa wapishi wa chakula ambacho kinapakuliwa leo tayari kwa kutumika katika soko la ajira.  Soko huru lenye mahitaji mbalimbali kwa sasa ikiwemo soko la kidigitali

Aidha, amewapongeza wazazi, walezi na wafadhili mbalimbali waliogharamia masomo ya wahitimu hao kwani uwekezaji huo uliofanyika umesaidia kuongeza mtaji wa watu katika taifa.

Na hivyo kuongeza uwezo wa kuzalisha, kukuza uchumi na kuboresha hali ya maisha ya wananchi wetu.

Kwa upande wa Mkuu wa chuo hicho Profesa Hozen Mayaya amesema chuo kimeendelea kufundisha kwa kutumia mitaala inayokidhi matakwa ya soko na inayozingatia umahiri.

Mitaala ya chuo huwapatia wahitimu wa elimu ya sekondari pamoja na vyuo vya kati fursa ya kujiendeleza katika fani mbalimbali za mipango ya maendeleo kuanzia ngazi ya astashahada hadi ngazi ya uzamili.

Prof. Mayaya

Zaidi ya wanafunzi 6000 wamehitimu katika chuo ambacho kimekuwa kikiboresha mfumo wa utoaji wa mafunzo mbalimbali kuendana na mahitaji ya soko .

 






Post a Comment

0 Comments