WATOA HUDUMA POSTA WATAKIWA KUWA NA SERA IMARA KUTEKELEZA UCHUMI WA KIDIGITALI

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

KATIKA  kutekeleza  mkakati wa kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara mtandao barani Afrika watoa huduma wa Posta  wametakiwa kuwa na Sera imara ya mpango wa utekekezaji  wa mahitaji ya miundombinu ya kuwezesha uchumi wa kidigital.

Akimuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakati akifungua  maadhimisho ya siku ya posta  Afrika ulioenda sambamba na semina kwa watoa huduma za posta Mkurugenzi wa Masuala ya Kisekta TCRA DKT Emanuel Manase   amesema  huduma za kiposta zinakuwa kwa kasi na kufungua fursa katika maeneo mbalimbali.

Dkt Manase amesema huduma za kiposta zinakuwa kwa kasi na kufungua fursa katika maeneo mbalimbali nchini.

Tanzania inakua mwenyeji wa maadhimisho haya ya siku ya Posta Duniani, kabla ya kufika katika kilele chenyewe taasisi za serikali Leo Jijini DODOMA zinajiweka katika hadhara ya Watanzania kueleza namna Shirika la Posta ambavyo limekua mgongo katika kuifungua nçhi kibiashara

Wakati akiyafungua Maadhimisho hayo Jijini hapa Dkt Manase anaona kuna umuhimu wa kuwapo kwa sera madhubuti na kuimarisha ushindani wa biashara barani Afrika.

Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ni "Mwezeshaji mahiri wa biashara ya mtandao  inayovuka mipaka barani Afrika"



 

Post a Comment

0 Comments