MZUMBE NA eGA WASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO

 ðŸ“ŒMWANDISHI WETU

CHUO Kikuu Mzumbe kimesaini Mkataba wa Makubaliano kuhusu ushirikiano wa Huduma za Kitaaluma na Teknolojia na Mamlaka ya Serikali Mtandao Tanzania (eGA) kwa lengo la kuendelea kuboresha huduma za Kitaaluma na Teknolojia zinazotolewa

Akizungumza wakati wa zoezi la kusaini makubaliano hayo Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha ameeleza kuwa sehemu ya Mpango Mkakati wa Chuo ni kuimarisha mifumo ya kidijitali na kuongeza wataalamu katika kutoa huduma za kitaaluma ili kuongeza idadi ya wanafunzi na kukuza ufanisi wa programu zinazotolewa na Chuo. Hivyo makubaliano hayo yatasaidia kubadilishana uzoefu na ujuzi kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Mamlaka ya Serikali Mtandao Tanzania (eGA).

Awali akizungumza wakati wa ufunguzi wa zoezi la kusaini mkata huo, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Eliza Mwakasangula, amesema makubaliano hayo ni matokeo ya Mkutano wa tatu wa TEHAMA uliofanyika Jijini Arusha kuanzia Februari 8 -12, 2023 ukiratibiwa na eGA.

Uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe umeona fursa na kupitia mradi wa Elimu ya Juu Kwa Mageuzi ya Kiuchumi upande wa Kujenga Ushirikiano wa Kazi na Sekta binafsi, Chuo Kikuu Mzumbe kimepata nafasi ya kuingia makubaliano hayo kwa maendeleo ya Taasisi na taifa

Dkt. Mwakasangula.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uwezeshaji katika Mamlaka ya Serikali Mtandao, CPA Salum Mussa, amekishukuru na kukipongeza Chuo Kikuu Mzumbe kwa hatua ya kuboresha na kuimarisha mashirikiano na kuwa miongoni mwa Taasisi za elimu ya Juu zinazoshirikiana na eGA moja kwa moja. Kwa niaba ya uongozi wa eGA CPA Salum Mussa, ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa ili kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa katika mkataba huo yanafikiwa.


Post a Comment

1 Comments