CWT YAPINGA UANZISHWAJI WA BODI YA TAALUMA YA WALIMU

 


📌HAMIDA RAMADHANI

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT)  kimetoa msimamo wake na  kukataa uanzishwaji wa Bodi ya kitaaluma ya Walimu  (Tanzania Teacher's Professional Board) kwa vile baadhi ya vipengele  katika sheria hiyo vinaoonekana  kumkandamiza mwalimu badala ya kumsaidia.

Akiongea na Waandishi wa habari leo Jijini Dodoma rais wa CWT  Mwalimu Leah Ulaya amesema mnamo mwaka 2019, CWT ilialikwa kutoa maoni kuhusu uanzishwaji wa Bodi hiyo lakini walitoa maoni yao kupinga bodi hiyo kwa vile haina tija kwa mwalimu.

" Kimsingi   tulikataa kwa nguvu zote baada ya kusoma Sheria hii tukajiridhisha  pasi na shaka kwamba Chombo hiki kililenga kumkandamiza mwalimu badala ya kumsaidia,". 

Na kuongeza kuwa" Tuliona wazi  majukumu yanaonyesha kwenye Bodi hiyo yanafanana na yale yanayofanywa na TSC (Tume ya Utumishi wa Walimu)iliyopo sasa," amesema rais  wa Chama hicho.

Aidha amesema mnamo tarehe 12 Aprili 2021 CWT ilialikwa na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukutana na kamati ndogo ya Bunge ya sheria kujadiliana kanuni za uendeshaji wa Bodi hiyo ambayo msingi wake ni sheria mama ambayo CWT imesema waliikataa tangu awali.

Amebainisha kwamba katika kikao hicho cha  tarehe 12 Aprili 2021 Chama cha walimu Tanzania kiliendelea  na msimamo wake wa usitishwaji wa chombo hicho  na kupendekeza kuimarisha utendaji wa TSC iliyopo sasa.



SABABU YA KUIKATAA BODI HIYO 

Mwalimu Ulaya amesema moja ya sababu ya wao kupinga uwepo wa bodi hiyo ni; gharama za uendeshaji wa Bodi hiyo kutegemea michango ya mwalimu (makato) kwa ajili ya usajili,Leseni na ada ya mwaka ambayo si chini ya Shilingi 50,000.

Pia amesema  katika Bodi hiyo kuna gharama za kusikiliza mashauri,gharama za semina ya kila  mwaka ambayo ni lazima kuhuisha Leseni hiyo na ikatokea mwalimu kashindwa kufanya hivyo atanyang'anywa Leseni na hivyo kupoteza sifa ya kufundisha .

Amesema hadi sasa kuna vyombo(mamlaka) zaidi ya vitatu vinavyosimamia mambo ya walimu hivyo kuongeza bodi ya walimu ni kumuongezea mwalimu gharama zisizo na msingi.

Tunataka kupunguza utitiri wa Vyombo vinavyomsimamia mwalimu. Mpango huo ni sawa  kumnyong'onyesha  mwalimu na kumuongezea  mwalimu mzigo mwalimu ambaye mshahara wake haumtoshi

Na kuongeza kuwa " Tunaomba wanachama na Walimu wezetu tuwe watulivi kwani Sisi Viongozi wenu wa kitaifa tumekwisha wasilisha msimamo wetu na mapendekezo yetu kwenye Kamati " amesema rais Leah.

Naye Naibu Katibu Mkuu CWT Maganga Japhet amesema Bodi hiyo haitajiki kwani TSC  haijasema kwa imeshindwa kuwasimamia walimu.

Amesema Bodi hiyo haina manufaa kwa Mwalimu zaidi ya kumdidimiza mwalimu kiuchumi na kimaendeleo.

Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa CWT  Deus Seif amesema  wao kama Chama wanaendelea kuipinga Bodi hiyo kwa maslahi ya mwalimu wa Tanzania.

Naye Makamu wa rais Dinah mathamani amesema msimamo wao wameshautoa na wanachosisitiza kwa sasa waache walimu kwani wanahitaji utulivu kwa kipindi  ili waendelee kufundisha watoto na kukuza elimu nchini.

Muajiri ndiye mwenye haki ya kumpeleka  masomoni au kujiendeleza kimasomo mwalimu na siyo mwalimu kujigharamia mafunzo tuendelee kuwa watulivu na kutiana nguvu ili kuinua elimu nchini


ANGALIA  ZAIDI KWENYE CPC TV👇👇👇



Post a Comment

0 Comments