UJENZI WA KITUO CHA HUDUMA YA PAMOJA MPAKANI (OSBP) WAFIKIA ASILIMA 67.

 


IMEELEZWA kuwa mradi wa ujenzi wa kituo cha huduma ya pamoja mpakani (OSBP) mpakani mwa Tanzania na Malawi eneo la Kasumulu unaojengwa na mkandarasi China Geo Engineering Corporation umefikia asilimia 67.1 na unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2021.

Hayo yamesemwa mkoani Mbeya na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa kituo hicho unaojengwa kwa awamu tatu na unagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 26.

Nitoe wito kwa mhandisi mshauri kuusimiamia mradi huu kikamilifu ili ukamililike kama ulivyopangwa kulingana na mkataba

Aidha, Naibu Waziri Kasekenya amesema kuwa mpaka sasa mkandarasi hana madai yoyote anayodai yatakayokwamisha utekelezaji wa mradi huo.

Mhandisi Mshauri wa Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Huduma ya Pamoja Mpakani (OSBP) katika eneo la Kasumulu kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi Daniel Mandari, akitoa taarifa ya mradi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho, mkoani Mbeya.


Mhandisi Mandari ameongeza kuwa mkandarasi amekwishakamilisha kazi za uandaaji wa ushindiliaji matuta ya karibu barabara zote na kwa sasa anendelea kukamilisha miundombinu ya mabomba ya maji safi, taka, zimamoto kabla ya kuanza tabaka la lami.

Kwa upande wake, Mhandisi Mshauri wa Mradi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi Daniel Mandari, amemueleza Naibu Waziri kuwa licha changamoto zilizoukabili mradi huo kuchelewa kukamilika, mkandarasi amekwisha kamilisha ofisi za wahandisi na maabara asilimia 100, ujenzi wa jengo la malori asilimia 80, Ghala asilimia 85, jengo la mifugo asilimia 84, jengo la abiria asilimia 81, geti namba 1&2 asilimia 75 na mizani asilimia 85.



Kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha huduma ya pamoja mpakani (OSBP) mpakani mwa Tanzania na Malawi katika eneo la Kasumulu kutakuza uchumi wa nchi zote mbili.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

 

Post a Comment

0 Comments