TPS SACCOS WATAKIWA KUWA WABUNIFU ILI KUFIKIA MALENGO

 


📌RHODA SIMBA 

KATIBU Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Christopher Kadio ameutaka uongozi wa chama cha TPS SACCOS kuwa wabunifu Katika uendeshaji na kuhamasisha wengine kujiunga ili waweze kufikia malengo ya pamoja.

Ameyasema hayo Leo November 18  jijini hapa wakati alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa Tisa wa Magereza SACCOS uliofanyika makao Makuu ya Jeshi hilo.

Aidha amesema kuwa viongozi hao wanapaswa kuwa wabunifu namna ya kuendeleza SACCOS yao hasa kwa kuzingatia dhana ya uzalishaji mali ikiwa ni pamoja na  kutoa elimu ya ushirika jambo ambalo litasaidia kuwa na maendeleo.

Niwapongeze sana kwa hatua hiyo na ili chama chenu kiweze kuendeshwa kwa tija lazima  kuzingatia sheria namba sita ya vyama vya ushirika ya mwaka 2015 hivyo simamieni hii sacos vizuri  

"Pia ungozi wa chama  niwasihi kwamba ili chama kiweze kufanya vizuri  lazima kipewe kipaumbele huku mkipaswa kuendana na kasi iliyopo hasa kutoa elimu ya ushirika,kushirikisha wanachama juu ya bajeti ya chama."alisema Kadio.

Nae Ramadhan Mbezi afisa mikopo wa chama cha TPS SACCOS amesema kumekuwa na mafanikio mengi huku  na  wanachama wakijivunia  chama hicho kupata mikopo Kwa wakati  ambapo mpaka kufikia oktoba mwaka huu tayari wanachama elfu 2,258 wamekopeshwa kiasi cha shilingi bilioni 3.3 Katika mkopo wa dharura.

Pia amesema tayari kiasi cha bilion 8 kimetolewa kwa wanachama 872 Katika mkopo wa maendeleo   jambo ambalo litanawasaidia kutatua shida zao kwa wakati.

Akielezea changamoto amesema hapo awali ilikuwa ni urejeshaji wa mkopo wa dharura lakini kupitia elimu ambayo wamekuwa wakiitoa na mfumo wa kupitia kwa mwajiri wao imesaidia kuondoa changamoto hiyo.

"Tuna mikakati mikubwa ni kuhakikisha wanachama wote wanajiunga ambao ni askari wastaafu na wenza wetu na kwa Sasa tuko elfu  11000 huku  Jeshi lina askari 12000 hivyo tunataka kuwafikia wote ili waweze kunufaika na SACCOS hii ambayo ina riba nafuu na kupata mkopo mkubwa ili waweze kutimiza malengo yao "amesema Mbezi.

Kwa upande wake mwanachama Hassan Rashid amesema kuwa Chama hicho kimewasaidia hasa Kwa upande wa faida kwani SACCOS imeleta fursa kwao ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za mikopo mbalimbali ambapo Wengi wamewezeshwa kujenga nyumba za kisasa na mambo mengine ya maendeleo.

Haya hivyo amewataka watu kuchangamkia fursa ya kujiunga kwenye chama hicho ambacho kitakuwa kichocheo kutatua shida zao kuliko kwenda kukopa nje ambapo kuna riba kubwa.

 

Post a Comment

0 Comments