JAMII FORUMS YAZINDUA USHIRIKIANO NA UMOJA WA KLABU ZA WAANDISHI TANZANIA


📌MWANDISHI WETU

UTPC na Jamii Forums wameingia katika Ushirikiano wa Kimkakati kwa lengo la kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari Nchini katika kuandaa Habari za Kiuchunguzi (IJ) na zenye Maslahi ya Umma (PIJ) ili kuchochea Uwajibikaji na utawala bora

Pia, Waandishi watajengewa uwezo kuhusu Usalama wa Kidijitali, matumizi sahihi na bora ya Vifaa na Mifumo ya Kidijitali na namna bora ya kutumia Uwanja wa Kidijitali kuendeleza kazi zao

Aidha, Mkurugenzi wa JamiiForums amesema litaanzishwa shindano la #StoriesOfChange litakalowalenga waandishi wa habari na washindi watatuzwa baada ya mchujo

Ushirikiano huu ni miaka 2, utaanza rasmi Januari 2023 na unaweza kuhuishwa baada ya kufanya tathmini

 



Post a Comment

0 Comments